skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane- Kigoma

Zaidi ya wananchi 100 kutoka kata ya Ziwani yenye vijiji vitatu vya Mtanga, Kalalangabo na Kigalye wamenufaika kiuchumi baada ya kufikiwa na nishati ya umeme kupitia mradi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Kata hiyo yenye kaya 600 na zaidi ya wakazi elfu 70,000 wamenufaika kiuchumi zaidi katika kijiji cha Mtanga ambacho kati ya vitongoji sita vilivyopo viwili tu ndio bado haijafikiwa na miundombinu ya umeme huku vijiji vya Kalalangabo na Kigalye zikiwa katika mchakato wa kuwekewa umeme baada ya usanifu kufanyika

Akizungumzia mafanikio hayo kwa wabia wa maendeleo waliotembelea katani hapo, diwani wa kata hiyo Zuberi Muftah amesema kabla ya umeme wageni walipangishiwa nyumba ya majani kwa shilingi kati ya 3000 -5000 na nyumba ya bati shillingi 7000-10000 kwa mwezi lakini baada ya umeme nyumba za majani zinapangishwa kati ya shilingi 7000-10,000 na nyumba za bati 10000-15,000, na hivyo kuwafanya wenye nyumba kuongeza kipato

Victor Labaa meneja wa uzalishaji wa umeme na masoko kutoka mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) akiwa na mkurugenzi mkuu Hassan Saidy wakitoa ufafanuzi kwa wananchi

“Kabla ya umeme vibanda vilivyopo sokoni vilipangishwa kwa shilingi 7000-10000, lakini baada ya umeme tunapangisha kwa shilingi 10,000-15,000 jambo ambalo limewanufisha

wananchi wengi na kuongeza muda wa soko kuisha kutoka saa 2:00 usiku ambapo mpaka kufikia saa 5:00 za usiku na watu kuongeza kipato zaidi kutokana na mzunguko mkubwa uliopo sasa” Amesema Muftah

Si hivyo tu amesema wavuvi walikuwa wakichaji betri zao zinazotumika kwenye uvuvi kwa bei ya sh 3000-3500 na wakati mwingine kuzipeleka Kigoma mjini ambapo iliwabidi kutembea kwa km 35 wakiwa majini kwa zaidi ya saa moja na hivyo kutumia muda mwingi lakini baada ya kupata umeme wanachaji kwa shilingi 2000 na kwamba wavuvi wameweza kuokoa takribani elfu 15 zilozotumika kuchaji kwa betri sipatazo 10 kila siku.

Zaidi ameeleza kuwa hapo awali kumbi zinazoonesha video zilitumia elfu 15,000 kwaajili ya kuendesha jenereta na sasa wanatumia gharama ya umeme wa 2000-2500 kuendesha biashara hiyo hali iliyofanya kumbi hizo kuongezeka mpaka kufikia 10 zilizopo sasa.

Pamoja na mafanikio hayo, Furaha Jamal mkazi wa kijiji cha Mtanga amesema kumekuwa na changamoto ya kukatika katika kwa umeme hata siku tatu mfululizo hali inayokwamisha shughuli za maendeleo na hasa kwa wavuvi wanaotegemea kuchaji betri kila siku kwaajili ya kuendesha shughuli zao na kuwaomba kuwapatia wataalamu watakaokuwepo katani hapo ili kutatua dharura na kutoa taarifa pindi hitilafu zinazopotokea ili wajipange zaidi badala ya kukaa kimya.

Naye Hassan Maulid amesema uwezo mdogo wa kiuchumi kwa baadhi ya wananchi ndio zababu ya wao kushindwa kuchangia gharama za kufungiwa umeme hata baada ya kuingizwa kwenye orodha ya wanufaika, na kwamba wapo baadhi ya wananchi waliowekwa kwenye umeme wa matumizi makubwa kuliko uwezo wao na kuiomba mamlaka kurejea taratibu zao kwani kuna wanaolipa elfu 5,000 wanapata unit 75 na wengine kwa pesa hiyo hiyo wanapata uniti 11 wakati uchumi wao unafanana nakuomba wote waingie kwenye matumizi madogo.

Mkurugenzi mkuu REA Hassan Saidy akitoa ufafanuzi kwa wananchi na kuwashukuru kwa kuunganisha umeme kupitia wakala wa Umeme vijijini.

Kwa upande wa wabia, Daniel Tiveau muwakilishi wa ubalozi wa Swiden nchini amesema maendeleo yanahitaji hatua na katika kuleta maendeleo kila mtu anawajibika, serikali inawajibika na wao kama wabia wanawajibika katika kuhakikisha wananchi wanapata mafanikio wanayostahili kwa kutoa fedha pamoja na kukagua shughuli zilizopswa kufanywa na pesa hizo.

Kwa upande wa Victor Labaa meneja wa uzalishaji wa umeme na masoko kutoka mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) amefafanua suala la malipo ya umeme majumbani kuwa tofauti kwa wananchi kwa kutoa ufafanuzi kwamba wanaotumia umeme chini ya uniti 75 kwa mwezi bei yao ni shilingi 100 kwa kila uniti na kwa wanaotumia zaidi ya uniti 75 wanalipia uniti moja shilingi 292 na kwamba watu hulilipa kulingana na makundi ya matumizi yao kama ya wafanyabiashara na viwandani.

Naye Joachim Ruweta meneja wa Tanesco mkoani Kigoma amewataka wananchi kutumia nguzo zilizowekwa ili kuongeza kipato serikalini fedha itakayosaidia kuongeza usambazaji na kwa wananchi wa maeneo mengine na kwamba kwa chanagamto zozote za umeme wasisite kutoa taarifa kupitia viongozi wao na kuwaahidi kuwa wataweka ofisi ndogo kwa vijana waliomaliza veta kwaajili ya kushughulikia dharura za kukatika kwa umeme katani hapo.

Kwa upande wa mkurugenzi mkuu wa REA Hassan Saidy amesema kitendo cha wananchi kujitolea nguvu na ardhi ili umeme uwafikie bila kudai fidia yoyote ni suala la kizalendo linalopaswa kuigwa na jamii nyingine kwa maendeleo endelevu.

This Post Has 0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma