skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

DKT. SAMIA MWENYE BARAKA! MOTISHA ZA MAMILIONI YAKE ZILIVYOCHAGIZA KUIFIKISHA YANGA FAINALI YA SHIRIKISHO BARANI AFRIKA-MWANA FA AONGOZA KIKOSI-MSIGWA MZIGO UPO HAUNA MBAMBAMBA

Anaaandika PhD. Ahmad Sovu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-kazi iendelee

Jana tarehe 17/5/2023 Klabu ya Yanga ya Tanzania imefanikiwa kufuzu katika hatua ya fainali ya michuano ya ngazi ya Shirikisho barani Afrika huku ikitajwa kuweka rekodi mpya na ya pekee hapa nchini katika medani za soka.

Hatua hii imetajwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa:

Yanga imeandika historia na kuipa nchi yetu heshima kubwa sana, kwa hakika hii ni heshima kubwa kwa nchi yetu na hata kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Makala haya ni mfulilizo wa makala yetu ya 3 iliyohusu motisha shawishi za Dkt.Samia Suluhu Hassan alizozitoa kwa Klabu za Yanga na Simba.

Motisha ilianza na Milioni 5 kila goli na baadaye Milioni 10 kwa kila goli.

Motisha hizi shawishi za Dkt.Samia Suluhu Hassan zimesaidia Simba kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika na hatimaye jana Yanga nayo wamefanikiwa kufuzu katika hatua ya Fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

Motisha za Mheshimiwa Rais Dkt.Samia
Kwa kutambua umuhimu wa motisha, hususan katika sekta ya michezo Dkt.Samia kwa mara kadhaa amekuwa akitoa motisha kwa timu zetu za Taifa na vilabu.

Dr. Samia suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na hii si kwa motisha pekee, lakini tumeona namna serikali anayoiongoza kupitia Balozi za Tanzania 🇹🇿 huko nje zilivyoonesha ushirikiano wa hali ya juu katika kuhakikisha timu zinakuwa salama na amani na zinafanikiwa kucheza michezo yake bila bughudha yoyote ile.

Mathalan, nchini Afrika Kusini tumeona ubalozi pamoja na mapokezi mazuri na uratibu uliandaa basi maalum la kuwapeleka Mashabiki watokao nchi jirani na Afrika Kusini kwenda uwanjani kuongeza nguvu ya kuisapoti timu yao.

Kama hiyo haitoshi, Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa katibu mkuu wake ndugu Saidi Yakubu ilitoa tikti 55 kwa kuwalipia mashabiki wa Tanzania kwenda Afrika Kusini kushuhudia mpambano huo ambao umezidi kuiweka Tanzania 🇹🇿 katika ramani nzuri zaidi ya michezo hususan katika anga za kimataifa.

Fauka ya hayo, Mheshimiwa Dkt.Rais Samia Suluhu Hassan alimridhia Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma maarufu mwana F.A kuungana na timu hadi Afrika Kusini hii ni hamasa kubwa sana kwa timu.

Kadhalika Jana majira ya mchana alipokuwa akihitimisha mazungumzo yake na wafabiashara wa Kariakoo Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliitakia Yanga Ushindi na akawataka Watanzania bila ya kujali tofauti zao za vilabu wakaipokee mara itakapofuzu kuingia hatua ya Fainali🇹🇿🇹🇿👏👏

Yanga imefuzu Mheshimiwa Majaliwa kasema ikapokelewe wewe na mimi ni nani tusiende kuwapokea wawakilishi wa Tanzania 🇹🇿 🤣🤣🤣

Kwa hakika huyu ndio Dkt.Samia Suluhu Hassan na mchango wake katika maendeleo ya soka la 🇹🇿.

Heko Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa motisha hii adhimu wewe ni mtu mwenye baraka.

Natija za kufuzu hatua hii

Mbali ya manufaa ya fedha ambayo Yanga wanapata kwa kufikia hatua hii zaidi ya Bilioni Moja na ushei pia hatua hii imepandisha Yanga katika ngazi mbalimbali kisoka na nchi kwa jumla.

Hatua hii pia imezidi Kuitangaza nchi Kimataifa katika maeneo mbalimbali ya dunia.

Pongezi kwa uongozi wa Yanga, mashabiki na Watanzania wote

Tunapenda kutoa Kongole na pongezi kwa uongozi wa klabu ya Yanga wakiongozwa na Rais wao Mhandisi Hersi Said na Mdhamini Gharib Said Mohammed maarufu GSM na wadhamini wenza wote, wanahabari, nyumba za habar na Watanzania wote kwa kuiunga Mkono Yanga ambayo ndio wawakilishi wa nchi yetu.👏👏👏

Ni imani yetu kuwa Mtazidi kuiunga mkono hatimaye kuutwaa ubingwa huo kabisaa dhidi ya U.S.M ALGER ya nchini Algeria 🇩🇿.

Kongole sana Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuonesha njia na jitihada katika kukuza na kuendeleza michezo yetu na kuitangaza nchi yetu.

Kwa kawaida yake huenda hii fainal akapanda dau tena🤣🤣🇹🇿🇹🇿 maana hana mbambamba chambilecho Gerson Msigwa, mnenaji wa serikali.

Mwandishi ni Mhadhiri na Mshititi kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kampasi ya Kivukoni DSM.

sovu82@gmail.com
0713400079

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma