skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Waandishi wa habari wa Mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma wametakiwa kutumia Takwimu za sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022  katika kuonesha Changamoto zinazowakabili wananchi pasipo kuogopa ili kuisaidia serikali kutatua Kero mbalimbali za kijamii nchini.

Hayo yamebainishwa na Kamisaa wa sensa Mheshimiwa Anne Makinda wakati wa semina ya Kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya uwasilishaji, usambazaji na uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ambayo imeandaliwa na Ofisi yaTaifa ya Takwimu

Makinda amesema mafunzo hayo kwa wana habari ni ya awamu ya 3 inayolenga kutoa elimu ya utambuzi wa matumizi ya matokeo ya sensa ikiwa ni baada ya  awamu ya pili uhesabuji wa watu na makazi kukamikika.

katika mafunzo hayo ya siku mbili waandishi wa habari 70 wamefundishwa namna ya kutambua takwimu na kuzitumia katika habari bila kuathiri uhalisia wake na hivyo kuleta chachu ya matumizi chanya ya takwimu kwa wanasiasa, wananchi, taariri na mashirika yanayoshirikiana na serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Picha ya pamoja kati ya waandishi wa habari na kamisaa wa Sensa Mh. Anne Makinda baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku mbili mjini Kigoma. Picha na Editha Karlo

Kwa upande wake Rais wa Muungano wa Klabu za waandishi wa habari nchini ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha waandishi habari Kigoma KGPC Deogratius Nsokolo amesema waandishi wa habari ni kiungo muhimu katika kuikumbusha serikali juu ya maendeleo ya eneo husika yaliyosahaulika.

Nsokolo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa serikali kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu hususani barabara zinazounganisha mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Katavi ambayo hadi sasa haijaunganishwa na barabara za kiwango cha lami

“Mikoa hii imechelewa mno kuunganishwa na miundombinu ya uhakika hasa barabara, tunatambua kuwa serikali inaendelea kuweka kipaumbele katika ujenzi lakini judi zaidi zinahitajika ili kukamilisha miradi hiyo hususani ujenzi wa barabara ya Uvinza hadi Mpanda ambayo kwa sasa haina mkandarasi, barabara hizi ni mhimu sana kwa ustawi wa wananchi wa ukanda wa ziwa Tanganyika.

ofisi ya Taifa ya takwimu inaendelea kutoa mafunzo na hamasa kwa waandishi wa habari kuhusu matokeo na matumizi sahihi ya takwimu ya sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2022.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma