skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu, Dodoma

Timu ya mpira wa minguu ya wasichana kutoka shule ya sekondari ya Fountain Gate ya Dodoma ambayo imetwaa ubingwa wa Afrika katika mashindano ya soka la wasichana kwa shule za sekondari, leo imealikwa bungeni na kupewa heshima kubwa na serikali pamoja na Bunge

Timu hiyo ambayo ilirejea mapema wiki hii kutoka Afrika Kusini yalikofanyika mashindani hayo, imeonesha umahili mkubwa na kuipa heshima Tanzania katika anga la Kimataifa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya wasichana ya Shule ya Sekondari Fountain Gate ya jijini Dodoma, Beatrice Charles  sh. milioni tano zikiwa ni zawadi yake kwa timu hiyo iliyotwaa ubingwa Afrika katika Mshindano ya Shule za Sekondari kwa Wasichana  katika hafla ya kuipongeza timu hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma, Machi 13, 2023. Kushoto niu Mkurugenzi wa Shule hiyo, Japhet Makau. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mafanikio hayo yanakuja wakati ambapo timu za Simba na Yanga nazo zikishiriki mashindano ya Club Bingwa Afrika kwa upande wa Simba na Shirikisho kwa upande wa yanga yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani afrika CAF huku zote zikiwa zimetina hatua ya robo fainali

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma