Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Na. Ashura Ramadhani
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Kazi,Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu ambae pia ni mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Prof Joyce Ndalichako, amefanya ziara ya kushtukiza kukagua ujenzi unaoendelea wa mradi wa maji Nyantale katika kata ya Nyansha wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Prof Ndalichako amesema kwamba, ziara hizo zinamsaidia kupata taarifa sahihi kuhusiana na mambo yote ya kimaendeleo ambayo ni muhimu na yana tija katika jamii kwani kuona ni kuamini na kuepuka kupewa taarifa zisizo sahihi kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo
Baada ya kushuhudia maendeleo ya mradi huo, amepongeza kasi ye utekelezaji na kuhimiza mkandarasi kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati, huku akimtaka meneja wa mamlaka ya mani RUWASA kusimamia kwa ukaribu miradi ya maji.
Aidha, meneja wa mamlaka ya maji Kasulu mjini Mhandisi Athumani Kilundumya amesema kwamba, tayari ameshampata mkandarasi ambae angeweza kutengeneza mifumo imara ya maji kwani kipindi cha masika huwa ni changamoto na tar 1/10 wanaamini wataweza kusaini nae mkataba, na itasaidia kupata maji safi zaidi ya kilomita elfu 7 huku akiishukuru serikali kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa mradi huo.

akitoa maelezo kwa mbunge kuhusu ujenzi wa mradi wa Maji Nyantare
Meneja amesema kuwa, kutokana kiwango cha fedha kilichopo kingeweza kuwasaidia kusambaza mabomba katika makazi ya watu, ili kuhakikisha kila sehemu ya makazi inapata maji kwa urahisi kwani wanaweza kufufua mifumo ya zamani ya usambazaji wa maji bila kusahau pia wana mikakati ya kuongeza mifumo mipya ambayo itaweza kuwafikia wananchi wengi na kwa haraka Zaidi.
Wakati huo huo, Prof Ndalichako ametembelea zahanati ya Nyantale pamoja na kituo cha afya Nyansha katika kata hiyo ili kujionea hali halisi ya huduma pamoja na miundombinu inavyoendelea, baada ya kuwakabidhiwa uongozi wa zahanati shilingi Million 100 za ujenzi pamoja na vifaa kwa ajili ya zahanati hiyo, huku akiwataka wafanyakazi kuwa na moyo wa kujitolea kwa kuihudumia jamii kwenye suala zima la afya.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, muuguzi wa zahanati hiyo Salome Samukole kwa niaba ya mganga mfawidhi, amesema zahanati ina jumla ya vyumba vitano ambapo chumba cha kwanza ni chumba cha mapokezi ya wagonjwa wanapofika, chumba cha pili ni kwa ajili ya kumuona Daktari, chumba cha tatu ni stoo ya dawa, chumba cha nne ni sindano na vidonda na chumba cha mwisho ni chumba cha kupumzika mama anapotoka kujifungua.