skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

kana na hatia na wengine kutokutwa na hatia. Hii inatokana na aina ya mashtaka yanayowakabili washtakiwa ambao wako katika makundi matatu kwa kuzingatia mashtaka yanayowakabili. Kwanza ni wale wanaoshtakiwa kwa makosa ya kufanya mkusanyiko na maandamano yasiyo halali. Pili wale wanaoshtakiwa kwa kutoa maneno ya uchochezi kwenye mkutano wa kufunga kampeni. Kundi la tatu ni wale wanaoshtakiwa kwa kufanya mkusanyiko na maandamano yasiyo halali. Washtakiwa wote katika utetezi wao walikana mashtaka na wengine walitoa utetezi unaoitwa kwa lugha ya kisheria “alibi” (alibai) kwamba hawakuwapo eneo la tukio, ilhali wakikabiliwa na mashtaka ya mkusanyiko na maandamano yasiyo halali. Lakini hata wale wanaokabiliwa na mashtaka ya uchochezi pia walikana kutoa maneno ya uchochezi huku wakidai kuwa yalikuwa ni maneno ya kawaida ambayo hayana tatizo. Kisheria wajibu wa kuthibitisha mashtaka ili kuwatia hatiani washtakiwa ni wa upande wa mashtaka. Katika kesi za jinai kama hii, kiwango cha kuthibitisha mashtaka ni kutokuacha mashaka yoyote. / Hii ina maana kwamba hata kama utetezi wa washtakiwa utakuwa dhaifu, kutiwa hatiani kutategemea uzito wa ushahidi wa upande wa mashtaka. Kwa hiyo upande wa mashtaka unapaswa uwe umethibitisha, kwanza washtakiwa waliokana kuwepo kwenye mkusanyiko na maandamano wanayodaiwa kuyafanya isivyo halali, kupitia ushahidi wa mashahidi wake na au vielelezo vya ushahidi walivyoviwasilisha mahakamani. Pia upande wa mashtaka unapaswa uwe umethibitisha kuwa washtakiwa walitoa maneno yanayodaiwa kuwa ya uchochezi. Hati ya mashtaka imebainisha maneno aliyoyatoa kila mshtakiwa yanayodaiwa kuwa ni ya uchochezi. Lakini kubainisha maneno hayo ni jambo moja na ni rahisi lakini kazi kubwa kwa upande wa mashtaka ni kuthibitisha kuwa maneno hayo ni ya uchochezi. Hapa vifungu vya sheria wanavyoshtakiwa navyo vitahusika sana ili kupata tafsiri ya uchochezi na kuona kama maneno hayo wanayodaiwa kuyatoa yanakidhi vigezo vya kisheria kuwa maneno ya uchochezi. Mbali na tafsiri hiyo ya vifungu vya kisheria, pia mahakama katika hukumu yake itakuwa imerejea hukumu za kesi mbalimbali zilizokwisha kuamriwa na au mahakama hiyo yenyewe au mahakama za juu yake zenye mazingira yanayofanana na kesi hii. Hivyo katika hukumu hiyo itachambua ushahidi dhidi ya kila mshtakiwa kuonyesha namna ulivyomgusa au kutokumgusa na kulinganisha na utetezi wake na hapa ndipo matokeo hayo / matatu yanaweza kujitokeza katika hukumu hiyo.

This Post Has 0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma