skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Busega 

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Michael Nome mwenye umri wa 42 amekutwa amejinyonga ndani ya mahabusu ya kituo cha polisi Mkula kilichopo wilayani Busega mkoani Simiyu, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni hasira na kutaka kukwepa mkono wa sheria.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda amesema kuwa marehemu  Michael Nome amegundulika kuwa amejinyonga akiwa mahabusu Januari 10 mwaka huu majira ya saa 12:30 asubuhi.

Kamanda Chatanda amesema marehemu alikuwa anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya fujo za mara kwa mara kwa mazazi mwenzake aitwaye Bahati Maduhu ambaye alifika kituo cha polisi kufungua jalada la uchunguzi. na mgogoro wa kifamilia na mzazi mwanzake aitwaye Bahati Maduhu kwa muda mrefu, na

“Na ukizingatia kwamba walitengana wakiwa bado wako kwenye umri wa kuhitajiana kwa kiwango kikubwa, kutokana na hali hiyo marehemu alikuwa akienda kwa mzazi mwenzake na kumfanyia fujo mara kwa mara ikiwemo kumpiga lakini pia na ugomvi wa aina nyingine.” anaeleza kamanda Chatanda na kuongeza kuwa;

“Familia ilijitahidi kufanya usuluhisi bila mafanikio na hatimaye Januari 8 mwaka huu majira ya saa tano usiku marehemu alikwenda nyumbani kwa mtalaka wake na kufanya fujo hali  iliyopelekea mtalaka huyo kufika kituo cha polisi na kutoa taarifa ya kufanyiwa fujo” amesema kamanda Chatanda

Inaelezwa kuwa wawili hao walifanikiwa kupata watoto tisa lakini kutokana na ugomvi wa mara kwa mara walilazimika kutengana japo mme bado alikuwa anampenda mkewe, kitendo kilichosababisha kila mara amfuate mkewe alikokuwa akiishi na kumfanyia fujo.

“Marehemu alikamatwa wakati jitihada za kumfikisha mahakamani zikiendelea alijinyonga kwa shati akiwa mahabusu na alifanikiwa kufanya jambo hilo kwa sababu kituoni alikuwa pekee yake hakukuwa na mtu mwingine, alitumia ile nafasi ya maandalizi ya makabidhiano ambapo askari waliokuwepo walikuwa wamejikita zaidi kwenye makabidhiano akatumia mwanya huo kujinyonga, wakati wanakabidhiana kimoja baada ya kingine ndio wakagundua mtu huyo amajinyonga” ameongeza kamanda Chatanda.

Katika hatua nyingine kamanda Chatanda amewataka  wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate sheria huku akiwashauri wanandoa kutumia mazungumzo kama namna ya kutatua migogoro yao

This Post Has 0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma