skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane- Kigoma.

Imebainika kuwa kutosomwa kwa taarifa za mapato na matumizi katika serikali za mitaa ni moja ya kero ambazo jamii mkoani Kigoma inazilalamikia na husababisha kuzorota kwa ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Kauli hiyo imetolewa  na  Mkuu wa dawati la elimu kwa umma, Leonida Mushema kwa niaba ya kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kigoma Stephen Mafipa wakati akitoa taarifa  ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia Aprili- Juni 2023 na kusema katika kata walizotembelea wamekutana na malalamiko hayo huku wananchi wakiomba kusomewa taarifa hiyo kwani ni haki yao kikatiba.

Amebainisha kuwa Wananchi wa  mkoa  Kigoma wamelaamikia tabia ya baadhi ya viongozi ya kutosoma taarifa ya mapato na matumizi  jambo ambalo linachochea ubadhilifu wa fedha za miradi ya maendeleo na vyanzo vingine vya mapato.

“Tuliwauliza baadhi ya watendaji kwanini hawasomi taarifa ya mapato na matumizi kwa wananchi, wakajibu ni kwakuwa wananchi hawafiki katika vikao na hata wakifika wanakuwa wachache licha ya kutokuwepo kwa nyaraka ziilzosainiwa kuonesha kuwa idadi ya wananchi waliofika haikutimiza akidi na vikao kushindwa kufanyika” Amesema Mushema.

Sambamba na hilo Mushema amesema katika kipindi hicho wameweza kubainisha miradi miwili  yenye thamani zaidi ya milioni 40, inayofanyiwa uchunguzi wa awali ili kubaini kama kuna ubadhilifu wowote uliofanyika ili hatua za kisheria zieweze kuchukuliwa.

Ameongeza kuwa miradi hiyo ipo katika shule ya sekondari Manyovu iliyipo wilayani Buhigwe ambapo mradi wa kwanza ni wa ujenzi wa matundu 12 ya vyoo wenye thamani ya shilingi milioni 13.2 ambapo imebainika kuwa fedha zimekwisha bila mradi kukamilika na  mchoro wa ujenzi haikuzingatiwa 

Mushema ameutaja mradi wa pili kuwa ni wa ukamikishaji wa ujenzi wa maabara wenye thamani ya shilingi milioni 30 ambapo ujezi huo umesimama bila sababu za msingi licha ya kuwepo kwa fedha  zaidi ya milioni nane, faili la nyaraka za matumizi ya fedha za mradi limepotea na mifuko 120 ya saruji imeganda.

” Tunahitaji kujua kwanini ujenzi hauendelei na kwanini vitu vinaharibika, ndio maana tumeamua kufanya uchunguzi wa awali ili atakayebainika kuwa amefanya ubadhilifu basi achukuliwe hatua za kisheria iili awajibike ipaswavyo” Amesema Mushemu.

Katika kipindi hicho (TAKUKURU) imefuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo sita yenye thamani ya bilioni moja na imeweza kuwafikia wananchi 12,671 katika kata 14 za mkoa huo kwa kufanya vikao ili kuibua kero na kuzifanyia kazi  ambapo jumla ya kero 208 ziliibuliwa na kero 137 zimetatuliwa huku kero 71 zinaendelea kufatiliwa.

This Post Has 0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma