skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Kadislaus Simon

Kijana mwenye umri wa miaka 20 mkazi wa Kijiji cha Kinazi Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ambaye jina lake tunalihifadhi, ametoa ombi kwa watanzania, serikali na hata wataalam wa magonjwa ya upasuaji kumsaidia kutatua changamoto aliyonayo ya kutokuwa na jinsia ili awe kama wanadamu wengine.

Akizungumza na Buha FM iliyomtembelea nyumbani kwaoo katika Kijiji cha Kinazi wilayani Buhigwe, binti huyo mwenye umri wa miaka 19 analalamikia kunyanyapaliwa na jamii pamoja na kukabiliwa na baadhi ya changamoto mbalimbali za kiafya

Mzee Petro Bahona ambaye ni Baba mzazi wa binti huyo, amesimulia kuwa baada ya kuzaliwa kwa binti yake na kujulikana kuwa hana sehemu ya jinsia inayomtambulisha kama msichana au mvulana walifanya jitihada za kumfikisha kwa wataalamu wa afya, na kwamba changamoto ya kifedha ilisababisha mwanaye kushidwa kupata huduma toshelevu juu ya suala hilo.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma maweni, Dkt. Lameck Mdengo ameeleza  kuhusiana na mtu mwenye hali kama hiyo kuwa, wanaouwezekano wa kupona na kwamba kwa sasa binti huyo anatakiwa kupata msaada wa kufikishwa katika hospital kubwa kaam Mhimbiri na Bugando ambapo anaweza kupata huduma kwa ukamilifu.

Imeshuhudiwa mara nyingi jamii kuwatenga watu wenye mapungufu fulani fulani ya kimwili lakini sivyo ilivyo kwa wakazi wa Kijiji cha Kinazi, ambao licha ya changamoto hiyo wao wanamuona kama watu wengine na kushirikiana naye kwa kila jambo la Kijamii.

Jamii inaombwa kumchangia mtoto huyu kifedha ilia pate matibabu ya uhakika kwa njia ya upasuajii utakaomuondolea simanzi na maumivu ya kiafya na kisaikolojia anayokabiliana nayo.

SIKILIZA SIMULIZI KAMILI HAPA CHINI

This Post Has 0 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma