skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki,Simiyu

Jamii mkoani Simiyu imetakiwa kuchukua hatua dhidi ya matukio/ majanga  ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao, watoto na mali zao

Miongoni mwa matukio/ majanga ambayo yametajwa yanaweza kuepukika ikiwa jamii itachukia tahadhari za haraka ni pamoja na ajali za barabarani,  majini, moto na migodini.

Hayo yamesemwa na kaimu kamanda mkoa, kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu Inspekta Faustin Mtitu ambapo amesema kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2022 jeshi hilo limekabiliana na matukio ya moto 21 na hakuna mtu aliyepoteza maisha.

Aidha amesema wamefanya uokoaji kwenye kwenye matukio 25 ambayo yanahusisha ajali za barabarani, migodi, mashimo ya vyoo, kusombwa na maji ya mvua, mabwawa na mito na yamesababisha vifo 43.

” Matukio hayo yamesebabisha vifo watu 43 wanawake 14 na wanaume 29 kwa upande wa majeruhi walikuwa 114 wanawake 38  na wanaume 76 na matukio yote kwa kipindi hicho hayakihusisha watoto wadogo” amesema inspekta Mtitu.

Katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu dhidi ya majanga Inspekta Mtitu amesema jeshi hilo kwa kipindi cha Januari hadi Disemba 2022 limeendelea kufanya jitihada za kuzuia majanga ya moto na majanga mengine yasitokee kwenye jamii kwa kufanya ukaguzi wa tahadhari na kinga dhidi ya majanga ya moto kwenye majengo na vyombo vya usafiri na usafirishaji, kuhakikisha miradi mipya ya ujenzi inapatiwa ushauri wa namna ya kuzingatia vigezo vya usalama kwenye majengo yote yanayojengwa mkoani hapo.

Inspekta Faustin Mtitu kaimu kamanda mkoa kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu akitoa elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi Somanda namna ya kukabiliana na majanga

Kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita ( 2022) majengo 1,537 na magari 76 yalikaguliwa, maeneo 88 yalipatiwa elimu na wanufaika walikuwa 24,754 wakiwemo wanafunzi wa shule za msingi kuanzia awali, na  elimu hiyo waliipata kupitia njia ya redio, kwenye  mashule, nyumba za ibada na kwenye mikusanyiko” amesema Inspekta Mtitu

Novemba 19 Mwaka 2020 watoto watu walipoteza maisha kwa kuzama kisimani kwa  nyakati tofauti katika kijiji cha Iwelimo kata ya Mwamanenge wilayani Maswa mkoani Simiyu mmoja alikuwa na miaka 2 mwingine miaka 3 wote wa kike.

Inaelezwa kuwa mazingira ya tukio hilo yalitokana na uzembe wa jami katika kaya yao kwakuwa walikuwa wanacheza nyuma ya nyumba ambapo kulikuwa na kisima ambacho hakijafunikwa na kujikuta wakidumbukia na hakuna mtu aliyejua mpaka walipoelea,

Annastazia Masanja ni mkazi wa KIdinda Bariadi amesema jeshi la zimamoto limewasaidia kupata elimu mbalimbali ikiwemo ya usalama barabrani na elimu wameifikisha hadi kwa watoto wao kwa kuwaelekeza namna bora ya kuvuka barabara waendapo shule na wakati wakirudi.

“Kiukweli mimi elimu niliyoipata kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji…nakumbuka siku moja  nikiwa mnadani  walifika wakatupa elimu kwasasa mwanangu mdogo ana miaka saba sahivi anajua namna bora ya kuvuka barabara kwa kuzingatia alama zilizopo barabarani kabla ya elimu hii alikuwa akienda shule kabla hajarudi tumbo joto ..na ukiangalia mimi ni mtafutaji uwezo wa kumsindikiza kila siku shuleni sina muda huo nipo naangaika kutafuta ridhiki kwaajili yake na ndugu zake” amesema mama huyo

Jisabu Masunga ni mkazi wa mjini Bariadi amesema ni vema sheria ikachukua mkondo wake ili kupunguza / kumaliza majanga hususan ambayo yanaepukika huku Veronika Mwobagulalila akisema bado elimu inatakiwa kwani wapo wanaofanya hivyo pasipo kujua madhara na wengine kuona madimbwi au visima vina manufaa zaidi pasipo kufikiria hatma ya watu hususan watoto wadogo ambao ndio wamekuwa wahanga wakubwa endapo wakidumbukia.

” Hivi mtu anachimba shimo alafu analiacha hivyo hivyo bila kulifukia unakuta jirani na eneo hilo kuna watoto wadogo sana wengine hata miaka mitano hawajafikia wanacheza karibu na eneo hilo mtu kama huyo bila sheria kuchukua mkondo wake makubwa yanaweza kutokea ….ni bora waoneshe mmoja wa mfano na wengine wataogopa na kuzingatia  nini sheria inataka” amesema Masunga.

” Wengine wanachimba mashimo kwaajili ya kukusanya maji hawana uwezo wa kuyajengea mi naona hapa kikubwa ni elimu kama mtu hana uwezo ni bora asichimbe kabisa na akikaidi akamatwe na shimo lifukiwe kwa nguvu ..lakini kuhusu ajali za barabarani na migodi kiukweli sheria isimame maana tunapoteza nguvu kazi” amesema Mwobagulalila   na kuongeza kuwa:

Miongoni mwa matukio yaliyoteka hisia za wananchi ni  pamoja na ajali za magari ikiwemo ya iliyotokea Januari 11,2022 iliyotokea eneo la Nyamikoma wilayani Busega mkoani hapa iliyosababisha vifo vya watu 15, ajali nyingine iliyotokea Marchi 27,2022 iliyotokea Kidurya wilayani Bariadi iliyohusisha vifo vya watu 7 na tukio la watoto watatu kuzama kwenye visima Novemba 19,2020 wilayani Maswa.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma