Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof Makame Mbarawa amewahakikishia Nwananchi wa mkoa wa Kigoma kuwa mradi wa ujenzi wa barabara inayoanzia kijiji cha Mnanila wilayani Buhigwe mpaka kijiji cha Kabingo wilayani Kakonko kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 260.6 utaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa.
Ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 300 ambapo amewatoa hofu wananchi na amesema kuwa serikali itahakikisha inakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa wakati uliopangwa.
“Kumekuwa na kauli za baadhi ya watu kuwa mradi utasimama , naomba niwahakikishie Raisi wetu Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha za utekelezaji wa barabara hii na changamoto kubwa ni upatikanaji wa saruji jambo ambalo linashughulikiwa na ujenzi utaendelea wala hautasimama” amesema Mbarawa
Waziri Mbarawa amesema wizara yake kwa kushirikiana na wizara zingine wataangalia namna nzuri ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara katika suala la msamaha wa kodi kwa baadhi ya vifaa vya ujenzi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi kwa wakati.
Hata hivyo amemtaka mkandarasi mshauri wa mradi pamoja na ofisi ya Wakala wa Barabara (TANROADS) Kigoma kuhakikisha wanasimamia kwa karibu ujenzi wa barabara hiyo ili ujenzi wake uwe na viwango vinavyokubalika na kukamilika kwa wakati kulingana na mkataba.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Kigoma Mhandisi Narcis Choma amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kwamba pamoja na changamoto za mvua kasi ya ujenzi iliyofikiwa inaendana na muda hivyo ujenzi huo utakamilika kwa wakati na kwamba wanachi wa mkoa wa Kigoma watakabidhiwa barabara hiyo ifikapo OCtober 23, mwaka 2023.
Akizungumza kwa upande wa wananchi, Elias Karova, dereva tax anayefanya safari zake Mnanila- Kasulu, amesema upatikanaji wa barabara ya lami utasadia kupunguza ajali pamoja na matumizi ya mafuta, na kuiomba serikali kuwatengenezea barabara za mchepuko wakati ujenzi wa barabara kuu ukiendelea ili kupunguza uharibifu wa magari yao
Mradi wa ujenzi wa barabara kutoka kijiji cha Mnanila mpaka wilayani Kasulu mpaka kijiji cha Kabingo wilayani Kakonko umegawanyika katika sehemu nne za Manyovu Kasulu km 68 chini ya Mkandarasi Zhejiang Communication Construction Group Co.Ltd (ZCCC), Kanyani Mvugwe km 70.5, mkandarasi wake akiwa SINOHYDRO Corporation, Mvugwe Nduta km 59.35 mkandarasi STECOL Corporation na Ndyta Kabingo chini ya mkandarasi China Henan International Corporation Group Co. Ltd (CHICO)
Imeandaliwa na Adela Madyane- Buha FM