skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Waziri wa elimu sayansi na tekinologia ambae pia ni mbunge wa jimbo la Kasulu mjini Prof. Joyce Ndalichako, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Radio cha Buha FM kinachoanzishwa mjini Kasulu mkaoni Kigoma

Akihutubia wananchi na viongozi wa asasi mbalimbali zilizoungana na shirika la OHIDE katika hafla hiyo, ameupongeza uongozi wa asasi ya OHIDE kwa kuanzisha kituo cha radio akitaja kuwa kitakuwa na msaada mkubwa wa mawasiliano kwa jamii mkoani Kigoma.

Profesa Ndalichako amesisitiza kuwa kuanzishwa kwa Radio mjini Kasulu ni suala la kupongezwa kwakuwa kitasaidia katika kuhamasisha maswala ya afya ikiwemo kuelimisha watu kijikinga na virusi vya korona na magonjwa mengine.

Mh. Profesa Joyce Ndalichako Mbunge, Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia akihutubia wakati wa uwekaji jiwe la msingi la kituo cha Buha Radio

Ameongeza kuwa kituo hicho kitakuwa ni chachu na muhimu sana katika mkoa wa Kigoma kwa ujumla kwa kuwa kitatumika katika kuhamasisha maendeleo katika jamii mbalimbali zinazopatikana mkoani humo ikiwemo wakimbizi kutoka nchi Jirani wanaoishi katika wilaya ya Kasulu na Kibondo kufahamu kuhusu masuala ya amani

Aidha Profesa Ndalichako ameelezea umhimu wa radio katika kutoa elimu juu ya maswala ya kilimo, mazingira, ulinzi na usalama, biashara na utetezi wa haki za makundi mbalimbali ili kusaidia kukuza ustawi wa mtu mmoja mmoja na nchi kwa ujumla.

Amewasihi wanachi wa wilaya ya kasulu kusikiliza vipindi mbalimbali vya radio vitakavyoanzishwa na kituo hicho cha kwanza kuanzishwa wilayani Kasulu.

Akisoma risala ya ujenzi wa kituo hicho, katibu wa asasi ya OHIDE Bi. Silesi Malli amesema, ujenzi wa kituo hicho umezingatia mahitaji ya jamii ya mkoa wa Kigoma katika sekta ya mawasiliano na Habari.

Bi. Malli amebainisha kuwa malengo ya BUHA ni kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha jamii kuhusu fursa mbalimbali za kimaendeleo na kuimarisha ushirikiano wa kijamii pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na maelewano baina ya wananchi na wakimbizi

Zaidi ya shilingi milioni 90 zimekwisha kutumiaka katika ujenzi huo unaotarajiwa kukamilika January mwaka 2022

Mwandishi. Evarist Kitungwa, Kasulu

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma