Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua Kamati ya…
Tanzania na India zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali hususani sekta ya elimu ili kuinua kiwancho na ubora wa elimu baina ya Tanzania na India yenye utajiri wa teknolojia ukilinganisha na Tanzania.

Hayo yamejadiliwa leo na Waziri wa Elimu wa Tanzania Profesa Joyce Ndalichako wakati akifanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania Bw. Shri Binaya Pradhan wakiwa katika maadhimisho ya siku ya kuenzi ushirikiano wa kiteknolojia na kiuchumi kati ya Tanzania na India yaliyofanyika tarehe 15/9/2021 jijini Dar es salaam

Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako amemshukuru Balozi Paradhan kwa namna nchi yake ya India inavyotoa ushirikiano mkubwa katika sekta ya elimu na teknolojia kwa tanzania ikiwemoo watanzania kuapata fursa ya elimu nchini India.
