Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka…
Na Anita Balingilaki, Simiyu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo anatarajiwa kuzindua mkakati rasmi wa kisekta wa mapambano dhidi ya kifua kikuu ambapo wizara mbalimbali zinashirikishwa katika mapambano hayo.
Hayo hayo yamebainishwa na mratibu wa kitaifa wa masuala ya uraghibishi, mawasiliano na uhamasishaji kutoka mpango wa taifa wa kifua kikuu na ukoma katika wizara ya afya Bw. Julius Mtemahanji huku akiongeza kuwa jambo jingine atakalolifanya mhe, Waziri Mkuu ni kukagua mabanda ya utekelezaji wa afua za kifua kikuu nchini.
Mkakati huo unatarajiwa kuzinduliwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kupambanana kifua kikuu duniani ambapo kitaifa utazinduliwa kwenye viwanja vya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Kuhusu sababu za maadhimisho hayo kufanyika mkoa wa Simiyu Mtemahanji amesema, mkoa huo unafanya vizuri katika harakati za mapambano dhidi ya kifua kikuu na kwa namna hiyo kama taifa linatambua mchango mkubwa wa mkoa huo na hivyo ni vema shughuli hiyo ikafanyika mkoani hapo.( Simiyu)
Mtemahanji amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasema ” kwa pamoja tunaweza kutokomeza kifua kikuu nchini Tanzania” kwahiyo ni wajibu wa kila mtanzania kuja pamoja katika kuhakikisha kwamba mapambano ya kifua kikuu yanafanikiwa.