skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Simiyu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya siku tatu kwenye wilaya za Itilima, Bariadi na Maswa mkoani Simiyu ambapo pamoja na mambo mengine atakagua shughuli za maendeleo na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi.

Ziara hiyo imethibitishwa na mkuu wa mkoa huo Dkt Yahaya Nawanda wakati akiongea na waandishi huku akiongeza kuwa mhe,Waziri Mkuu Marchi 24, 2023 atakagua miradi miwili na kuongea na wananchi wilayani Itilima, Video hii hapa chini inafafanua kwa kina kuhusu ziara hiyo na mtendaji mkuu wa serikali.

Awali Dkt Nawanda amesema mhe,Waziri Mkuu anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani ambapo kitaifa yatafanyika Marchi 24,2023 kwenye viwanja vya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani hapo.

Marchi 26, mhe, Waziri Mkuu baada ya kukamilisha ziara yake ataelekea mkoani Shinyanga kwenda makao makuu ya nchi jijini Dodoma.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma