skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane- Kigoma

Baadhi ya watoto wa shule ya msingi Mvugwe iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma wamewaomba wazazi kutohifadhi picha na video za ngono katika simu na flashi majumbani kwaajili ya kulinda maadili yao.

Si hivyo tu,wameiomba pia jamii kutoonyesha video hizo katika kumbi za video hususani zinazoonesha mpira pamoja na maigizo nyakati za usiku kuanzia saa mbili.

Akizungumzia hilo January Kiza (sio jina lake halisi) mwanafunzi wa darasa la tano kutoka shuleni hapo amesema kwa mara ya kwanza aliona video hizo kwenye simu ya mama yake alipomuagiza kwenda kuchaji kwenye vibanda vya kuchajia simu na baadae kuona kwenye flash ya nyimbo za kwaya inayotumiwa na kila mwanafamilia nyumbani kwao.

Naye Zebedayo Yasini ( sio jina halisi) amesema aliona video hizo kwenye simu ya kaka yake ambae nyakati za usiku huwa anakaa na simu yake akiwa na rafiki zake wakijifanya wanasoma kumbe wanaangalia video za ngono.

Akizugumza kumbi za video Farida Medebe (sio jina halisi) amesema huwa kuna matangazo maalum kama ya “pilau” na kwamba jina hilo linaashiria kuwa siku hiyo kuna video hizo zitaoneshwa na wengi wao hujitokeza kuangalia

Katika utafiti wa ndani uliofanywa na mwandishi katika sekondari ya Makere iliyopo kata ya Makere wilayani Kasulu wanafunzi 300 walikiri kuona video hizo huku wengi wao wakiziona kwa wazazi au ndugu wakaribu kupitia simu zao na kusema kuwa zinaharibu saikolojia yao pindi wanapokuwa darasani

Wakizungumzia hilo baadhi ya wazazi Amando  Ndondeye mzee maarufu kutoka kijiji cha Mvugwe amekiri watoto kuathirika kimaadili kutokana na video hizo na kuziomba mamalaka za serikali zihusike katika kuzuia mitandao inayorusha video hizo kwani zinapatikana zaidi kwenye mitandao kupitia simu ganja

“Ni wazi kuwa zipo mamlaka zinazofuatilia maudhui ya vitu vinavyorushwa nchini, ni vema waziri mwenye dhamana akashughulikia masuala hayo na kuzuia kwenye chanzo na kukifungua ili kunusuru maadili ya watoto wetu kwakuwa yanamomonyoka kila siku”amesema Ndondeye

Naye Alex Vyuguseka mtendaji wa kata ya Mvugwe amesema athari za video hizo majumbani zimeshaanza kuonekana ambapo kumekuwa hakuna heshima baina ya wazazi na watoto huku watoto wakiwa makini zaidi na simu au video na tamthiliya siszokuwa na maadili na kuonekana kuzifurahia

Akizungumzia hilo Hawa Abdala mjumbe wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWA)ameiomba serikali wilayani Kasulu kufanya ufuatiliaji kwenye vibanda vya video pamoja na vibanda vya kurushia video  kwakuwa mara nyingi watoto huzunguka maeneo hayo nyakati za usiku hadi saa nne  wakiwa wanaangalia tamthiliya za Erturgru zinazorushwa na television ya Azam.

Kwa upande wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mvugwe Marystella Ndigize amesema pamoja na video za ngono zipo changamoto nyingine zinazowakabili watoto ambayo ni masoko ya usiku yanayosababisha baadhi ya watoto kutaka kufanya kwa vitendo yale waliyoyaona kwenye simu za wazazi wao na hatimaye kuharibu maendeleo yao kielimu.

Akizungumzia hilo Bakari Bussoro afisa ustawi wilaya ya Kasulu amesema suala la watoto kutazama video za ngono ni ukatili usiopaswa kufumbiwa macho na kwamba  waliunda mabaraza ya watoto ili kuwaelimisha juu ya haki zao pale inapotokea ukatili sambamba na kuunda kamati za MTAKUWA kwenye kila kijiji kwaajili  ya kuhakikisha unyanyasaji unapungua kwa watoto huku akitaja kikwazo kuwa jamiii katika kutoa ushirikiano wa uendeshaji wa kamati hizo.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma