Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Na. Felister Nestory Matinde -Mwanza
Katika kuelekea kilele Cha siku ya familia duniani ambayo huadhimishwa Mei 15 kila mwaka, jamii imeshauriwa itambue haki za watoto na wanawake ambao wamekuwa ni daraja la kufanyiwa vitendo vya ukatili.
Wito huo umetolewa na Mkurugenz mtendaji wa taasisi ya Haki Zetu iliyopo Nyasaka wilaya ya Ilemela jiji Mwanza Bw. Gervas Evodius wakati wa mahojiano maalumu na Buha FM Jijini Mwanza kuelekea uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya familia
Akijibu hoja kuhusu watoto wengi kuishi katika mazingira hatarishi jijini Mwanza na sababu za wazazi wao kutowachukua, Bw. Evodius ametaja kuwa migogoro mingi isiyotatuliwa kwa wakati katika familia ni chanzo cha ongezeko la watoto wa mtaani na amesisitiza kuwa jamii inatakiwa iachane na ukatili unaofanywa dhidi ya watoto na wanawake na jamiii pia kutambua haki ya mtoto wa kike.
Bw. Evodius amesema kuwa ukatili huo unaanzia katika ngazi ya familia kwenda kwenye jamiii hali ambayo inatishia maisha ya wanawake na watoto kwa ujumla na kusababisha kutokujiamini na kupunguza upendo ambao ndio msingi wa familia.
“Sisi Kama taasisi ya Haki Zetu ambayo inajihusishana kutetea Haki za watoto vijana na wanawake Mara nyingi tumekuwa tukikutana na visa lakini wakati mwingine inakuwa ni vigumu kuchukua hatua za kisheria sababu Kuna wazazi wengine wanapoteza ushahidi pamoja na kuelimisha jamii kuhusu vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto na wanawake na jamii kutokufumbia macho vitendo hivyo viovu”amesema Director Evodius.
Imeelezwa kuwa sababu za ukatili ikiwa pamoja na mlengwa kupitia ukatili zinatokana kulipiza kisasi,mabadiliko ya technolojia na mwingiliano wa tamaduni za magharibi hali ambayo inayochochea vitendo vya ukatili na unyanyasaji.
“Tunao vijana 190 kwenye shule tofauti na kutoka mikoa mbalimbali Kama shinyanga,geita na Mwanza ambao wanaishi kwenye mazingira magumu na tunawapatia elimu, tunawalipia ada pamoja na kuwalipia bima za afya ambayo lengo ni kusaidia familia na kuwapa mitaji midogo midogo halli ambayo itasaidia kujikwamua kiuchumi” amesema Mkurugenz Evodius.
Hata hivyo ameihasa jamii kuachana na vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa viikitishia maisha ya watoto na wanawake,jamii inatakiwa ivunje ukimya unaofanywa na baadhi ya watu,kubadilisha baadhi ya sheria ya ndoa hii itasaidia wanawake na watoto watapata Haki zao na kujua nini Cha kufanya baada yakufanyiwa ukatili pamoja na jamii iachane Mila potofu za kuozesha watoto wadogo huku wakijua ni kinyume Cha Sheria.
Sambamba na hayo amesema kuwa afya ya uzazi kwa watoto wa kike na akina mama ni muhimu kuwapa elimu ya uzazi hii itasaidia kuondokana na mimba zisizotarajiwa pamoja na watoto wa kike kubeba mimba chini ya umri wa miaka 18 Hali ambayo ni tishio kwa afya zao.
Wakati huo huo shirika la hilo limeiomba serikali kupunguza gharama za taulo za kike kwa kuweka mkakati wa kusaidia watoto wasichana wakiwa shuleni ambao wanatoka kaya maskini pamoja na kuwajengea chumba maalum kwa ajili ya kubadilisha taulo za kike shuleni.
Watoto kadhaa waliohojiwa na Buha FM jijini Mwanza kuhusu sababuu za kuishi mitaani katika mazingira hatarishi walitaja kukimbia madhira ya ugomvi baina ya wazazi wao, umaskini pamoja na kukosa upendo miongoni mwa wana familia ikiwemo ushawishi wa kwenda kupata maisha bora mijini.
Kwa upande wake hussen sultan mkazi wa Mecco mwenye umri wa miaka 26 anasema kuwa kilichompelekea kukimbilia mtaani ni kufukuzwa nyumbani na ndugu baada ya wazazi wake kufariki dunia.
Nae fidelis Amos mkazi wa Mugumu Serengeti mwenye umri wa miaka 13 amesema kuwa kilichompelekea Kuja mtaani ni baada ya baba yake kuachana na mama yake na kuolewa na mume mwingine ambaye amekuwa akimfanyia ukatili na kukumbilia kwa Bibi ambako alikosa mahitaji ya msingi na baadaye aliamua kwenda mjini ambako anaishi bila makazi maalumu.

Kwa upande wake Bi. Martha Felician mkazi wa Mecco jijini Mwanza amesema wasichana wengii wanaingia katika majukumu ya kifamilia kutokana na kufanyiwa vitendoo vya ukatilii ikiwemo mimba za mapema na ndoa za utotoni ikiwa ni pamoja na kubakwa.
Akitoa ushuhuda Bi. Martha anabainisha kuwa alipata mimba katika umri mdogo suala lililopelekea wazazi kumfukuza nyumbani na kuishi maisha ya shida kutokana na ukatili aliyofanyiwa mpaka kubeba ujauzito ambao umezima ndoto zake.
“Ninawaomba wazazi msiwatenge watoto wenu pindi wanapopata mimba katika umri mdogo badala yake wapatieni msaada wa elimu au msaada wa kifedha ili waweze kujikimu katika maisha hii itapunguza kuwa tegemezi, Alisisitiza Martha Felician.