skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limeanza mchakato wa kuinua ubora wa elimu kwa kuongeza ushiriki na ufaulu wa Watoto wa kike katika masomo ya sanyansi na hisabati

Hayo yamebainishwa na Mheshimiwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ndugu Angela Kairuki katika hotuba yake iliyosomwa na kaimu afisa elimu mkoa wa Kigoma Bw. Shukuru kalegamye wakati wa kufunga kongamano la wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi na hisabati kwa shule za sekondari kwa mikoa ya Kigoma, Songwe na Tabora lililofanyika mjini Kasulu mkoani Kigoma

Ndugu Kairuki amesisitiza kuwa Serikali ya Tanzania imeseka msukumu maalumu ukwa wasischana kusoma masomo ya sayansi na hisabati na kwamba uanzishwaji wa midahalo kwa wanafunzi na walimu wa Sanyansi ni sehemu ya mipango ya kutambua changamoto, vikwazo na kufahamika kwa fursa zilizopo katika masomo hayo kwa watoto wa kike.

Amebainisha kuwa serikali tayari imeanza kuzitambua changamoto ambazo ni vikwazo ikiwemo baadhi ya wazazi kuwashawishi watoto kutosoma masomo hayo, walimu kukosa mbinu rafiki na shirikishi pamoja na kasumba ya jamii kuona kuwa masomo ya sayansi ni magumu na kwamba wasichana hawayawezi ukilinanisha na wavulana.

“Natoa wito kwa jamii, wazazi na wanafunzi wenyewe wahamasike na wapende kusoma masomo ya sayansi na sisi tuitaendeleza kuwawezesha walimu kwa kuwajengea uwezo ili wawe na maarifa ya kutosha ya kufundisha masomo ya sanyansi” imesema sehemu ya hotuba ya waziri wa TAMISEMI Angela Kairuki.

Viongozi na wanafunzi walioshiriki kongamano la Sayansi na Hisabati mjni Kasulu, kutoka kulia ni Ayoub Kafyulilo (afisa kutoka UNICEF), Dr. Bugogo kutoka TAMISEMI, Mwl. Shukuru kalegamye kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa, Asha Mbwambo kutoka Wizara ya elimu na mwisho ni mkuu wa Chuo cha Ualimu Kasulu

Mheshimiwa Kairuki ameagiza watendaji wote wa serikali, maafisa elimu na wadau wengine kushirikiana kutekeleza mikakati yote ya kuwezesha Watoto wa kike kusoma masomo ya sayansi na hisabati sambamba na kusimamia mpango wa kila mtoto wa kike anayebarehe asome unafanikiwa.

Kwa upande wake mtaalam wa elimu kutoka UNICEF Bw. Ayoub Kafyulilo amepongeza serikali kwa kushirikisha umoja wa mataifa katika kutekeleza mpango huo ambao utazalisha wanasayansi, tekonolojia na uhandisi kwa watoto wa kike.

Amesisitiza kuwa maoni na ushauri wote uliotolewa na wakufunzi pamoja na Watoto wenyewe ni msingi mzuri kwa shirika hilo pamoja na wadau wengine ili kukamilisha utafiti wa nini ni kikwazo cha Watoto wa kike kutosoma masomo ya sayansi na hisabati yanatafutiwa ufumbuzi.

Kwa upande wao Watoto hao kutoka mikoa ya Songwe, Kigoma na Tabora waliweka bayana katika mdahalo wao kuwa, wasichana wengi hawasomi masomo ya sayansi kutokana na kukatishwa tamaa na jamii pamoja na walimu.

Walibainisha kuwa, baadahi ya wazazi hawawaoni umuhimu wala hawawahimizi Watoto wao wa kike kutokana na dhana tu kwamba masomo hayo ni magumu na kwamba wavulana pekee ndio wenye uwezo wa kusoma, huku wengine wakitaja kuwa uchache wa walimu wa sayansi na ushawishi hasi wa shuleni ni moja ya vizuizi.

Awali mwakilishi wa TAMISEMI Dr. Yangson Bugogo alibainisha kuwa mdahalo huo wa wanafunzi kuhusu masomo ya sanyansi na hisabati kwa mikoa ya Songkwe Kigoma na Tabora ni hatua za awali za utekelezaji wa mpango wa kuhakikisha Watoto wakike wanasoma masomo hayo kufuatia kuwepo kwa matokeo ya awali ya tafiti zilizoonesha kuwa wasichana wako nyuma ukilinganisha na wavulana.

Kwa mujibu wa taarifa za wizara ya elimu nchini Tanzania kiwango cha ufaulu kwa wasicha katika mikoa hiyo kilikuwa chini katika masomo hayo kwa wastani wa asilimia kati ya 15 hadi 88 nyuma ya wavula kwa mkoa wa Kigoma,

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma