Na. Ashura Ramadhani Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Kazi,Vijana, Ajira na watu wenye…
Waandishi habari kutoka mikoa ya Kigoma, na Dar es Salaam, wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi yenye ukubwa wa 4,471km iliyopo mkoani Katavi iliyoanzishwa mwaka 1974 kwa lengo la kutafsiri mafunzo waliyopata ya uandishi wa habari za mazingira kwa vitendo
Miongoni mwa mambo waliyojifunza ni masuala ya uhifadhi na ulinzi wa mazingira, Wanyamapori na shughuli za utalii ambazo ni kiini cha shughuli za kila siku cha hifadhi za taifa.
Sambamba na hilo waandishi hao wamejifunza namna mabadiliko ya tabia nchi yanavyoweza kuathiri ustawi wa wanayama pori na mali asili zilizopo mbungani, ushirikishwaji wa jamii katika ukusanyanji na uchakataji wa habari na uwasilishaji.
Katika ziara hiyo, wanahabari walishuhudia hali mbaya ya ukame, kilimo katika eneoo la hifadhi, makazi ya watu jjirani na hifadhi sambamba na ukame ambaoo unaathiri ustawi wa wanyamapori hususani Viboko unaotajwa kusababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mfano, ziwa Katavi ambalo kwa kipindi hiki lilitakiwa liwe limefurika kwa maji, mpaka sasa maji hayajaongezeka kutokana na uchache wa mvua uiliopo kwa mwaka huu hali inayoashiria hatari pia kwa ustawi wa wanyama hasa viboko wanaotegemea maji ili kuishi sambamba na wanyama wengine ambao hulitumia Ziwa katavi kwa ajili ya maji ya kunywa wakiwemo Twiga, Nyati, Tembo na Simba

Baada ya kushuhudia madhara ya uharibifu wa mazingira na uwepo wa viashiria vya athari za mabadiliko ya tabia nchi, Wandishi hao wanatoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza mazingira kwani kwa kukata miti na kuharibu vyanzo vya maji, tunatengeneza bomu ambalo litatulipukia wenyewe
Matembezi haya yamedhaminiwa na shirika la Good Haverst organisation, Ohide pamoja na Buha Fm Radio baada ya mafunzo ya siku moja ya uandishi wa habari za mazingira kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora ambayo ni sehemu ya mpango na ufadhili kutoka taasisi ya WAN-IFRA na Media Freedom zinazolenga kujenga uwezo wa waandishi wa habari na taasisi za kijamii katika kuzingatia taaluma na kuandika habari zinazohimiza utunzaji wa mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Mwandishi: Adela Madyane
Mhariri: Prosper Kwigize