skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Changamoto ya miundombinu afya pamoja na mwamko hasi wa jamii kuhudhuria kliniki na wajawazito kujifungulia nyumbani kunatajwa kuwa chanzo cha maelfu ya vifo vya wanawake nchini Tanzania. Mwandishi wetu Prosper kwigize amefuatilia takwimu za vifo na kutuandalia ripoti ifuatayo kutoka Kigoma

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na UNFPA pamoja na WHO, Wastani wa wanawake 30 hufariki dunia kila siku nchini Tanzania kutokana na matatizo ya ujauzito na uzazi, wakati mkoani Kigoma kwa kipindi cha mwaka 2022, jumla ya vifo 102 vinavyotokana na uzazi viliripotiwa, na tangu  Januari 2023 hadi sasa jumla ya wanawake 26 wamefariki kutokana na sababu hiyo.

Akimzungumzia sababu ya vifo vya wagonjwa na wajawazito  kaimu mwakilishi wa WHO nchini Tanzania Dk Nemes Iriya amesema, changamoto kubwa ni mfumo dhaifu wa rufaa ndiyo maana wameamua kuchangia magari ya wagonjwa ili kuimarisha usafiri ili iwe rahisi kutoa rufaa kila matatizo yanapotokea kwa mama mjamzito

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa magari mawili ya kubebea wagonjwa yenye thamani ya shilingi milioni 175 kusaidia mpango wa dharura wa miaka mitatu unaolenga kuboresha huduma za afya na kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wajawazito na watoto. Aidha WHO imetoa mashine za kuchunguza magonjwa ili kutoa matibabu ya uhakika kama anavyoelezea tena Dr. Iriya

Wananchi wamekuwa na maoni tofauti kuhusu usaidizi wa umoja wa mataifa kwa serikali ya Tanzania katika kuokoa Maisha ya wanawake na Watoto

Wananachi wa mkoa wa Kigoma waliowakilishwa na Odiria Sunzu mkazi wa Kasulu wanakiri kuwa ujio wa misaada ya kiafya hasa usafiri ni ukombozi kwao kutokana na kwamba wamekuwa wakipoteza ndugu zao pindi wanaposafiri umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za uzazi na ukunga hasa nyakati za usiku

Tulikuwa tunasafirisha wagonjwa kwa shida sana, tulikosa magari na kulazimika kutumia pikipiki na baiskeli nap engine kwa kutembea kwa miguu, na baadhi ya wanawake walijifungulia njiani hali iliyoleta adhan a vifo, tunashukuru UN na serikali kwa kutambua mateso yetu” amesisitiza Odria ambaye pia ni kiongozi wa wanawake

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye akipokea misaada hiyo kutoka WHO na UNFPA amepongeza mashirika hayo kwa juhudi za kuiunga mkono serikali katika utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto na kujenga uwezo wa serikali na watumishi

Tanzania inatajwa kuwa muongoji mwa nchi ambazo maisha ya wanawake wajawazito na watoto wachanga yako hatarini zaidi ukikinganisha na makundi mengine.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma