skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Ujio wa kituo cha radio cha kijamii kinachorusha matangazo yake katika wilaya ya Kasulu imetajwa kuwa ni moja ya suluhisho la changamoto za mawasiliano ya umma mkoani Kigoma.

Hayo yamebainishwa na Mariam Rafael, Mwanamke Mkazi wa Kasulu, mjasiriamali katika soko la Mnadani, yeye ambaye ni miongoni mwanawake wanao pambana kufanya biashara ndogondogo ili kuhakikisha watoto wake wanapata mkate wa kila siku.

Katika Makala maalumu iliyoandaliwa na  Mussa Milanya kutoka kituo cha Buha FM, Wanawake wamekiri kukabiliana na changamoto nyingi za kijamii ikiwemo za kutopata huduma stahiki kutoka kwa wanandoa wao, jambo ambalo anaona linapaswa kujadiliwa na vyombo vya Habari hususani Radio.

Mahojiano na wananchi wa Kasulu kuhusu changamoto za maisha na umhimu wa Radio wilayani Kasulu

Waswahili wanasema Tembo haelemiwi na mkonga wake, hivyo ndiyo ilivyo kwa Mwanamke huyo, anayewakilisha kundi kubwa la wanawake nchini, ambao wanabeba mzigo mkubwa wa kulea watoto huku wenza wao wakiwakimbia kwasababu mbalimbali na sababu kubwa ikitajwa kuwa ni ugumu wa maisha kama anavyoeleza.

Festus Faustine ni kijana mkazi wa eneo la Kwashayo kasulu, anasema kuanziswa kwa Radio Buha fm, kutawaibua vijana wengi wenye vipaji na ambao wanandoto kubwa katika Sanaa.

Wafanyabiashara ambao ni wananchi wa Kasulu, wameushukuru uongozi wa Buha Fm kwa kuanzisha kituo cha kwanza cha Redio katika Wilaya ya Kasulu, huku wakizidi kuuomba uongozi wa Buha kuhakikisha radio inaendelea na kuwa sauti ya wananchi hao.

Redio Buha fm, ni radio ya jamii inayopatikana katika eneo la Mwilamvya Wilaya ya kasulu huku lengo kubwa la kuanzishwa kwa Redio hiyo ni kuwa sauti ya wananchi wa Kasulu, kupitia masafa ya 100.1 fm.

Makala haya yameandaliwa na MUSSA MKILNAYA NA PALMER AYUBU

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma