skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Felister matinde Nestory, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mhandisi Robert Gabriel amewataka machinga wote mkoa wa Mwanza kutii Sheria na taratibu kwa kurudi katika maeneo waliyopangiwa.

Mhandisi Gabriel sema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa machinga wote wanatakiwa kurudi katika maeneo waliopangiwa hii inatokana na baadhi ya machinga kurudi maeneo ambayo sio rasmi.

Ndani ya siku chache machinga wameanza kuvamia mji wa Mwanza na kukiuka utaratibu na pia kuna wakwepa Kodi ambao Wana kundi la vijana ambao wanawapa bidhaa na kukosesha serikali mapato pia biashara kufanyika kihorera vijana hao wamekuwa wakizorotesha zoez Zima la kulipa kodi“amesema Gabriel

Aliongeza kuwa machinga atakaye kamatwa akifanya biashara maeneo ambayo sio rasmi atachukuliwa Sheria na adhabu zitatolewa kwa mujibu wa Sheria na ukamataji utafanyika kwa mujibu wa sheria.

“Kuna baadhi ya makundi ya uchochezi yanasema kuwa Mkuu wa Mkoa kasimamisha mgambo kwa hiyo Sasa hv tufanye biashara barabarani tuvunje Sheria mgambo hawatatugusa Tena twendeni tukavamie kila mahali jambo hilo hakuna kabisa duniani kote utawala wa Sheria unazungumza kutii Sheria na kuwajibika hivyo serikali haitakaa kimya wazee na viongozi wa dini wameniomba wamenambia Mkuu wa Mkoa,Mkoa unavurugika” amesema mhandisi Gabriel.

Hata hvyo aliwataka machinga kujenga vibanda maeneo yaliyokubalika na  kutengwa na serikali ili kuondoa usumbufu katika hifadhi ya barabara.

Kwa upande wake katibu Mkuu shirikisho la umoja wa  machinga Taifa Bw. Venatus Anatory amesema kuwa Kama Shirikisho la umoja wa machinga hawajapata malalamiko Kama Kuna machinga wamekosa maeneo hivyo amewaomba machinga kwenda maeneo waliyokubaliana sababu suala la machinga ni endelevu na kuwasihi kushirikiana na viongozi katika kutii Sheria bila shuruti.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma