skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory, Mwanza

Wanachama wa Vikundi vya akina mama ,vijana na watu wenye ulemavu ambao wamehama Mkoa wa Mwanza bila kurejesha fedha za Mkopo wa 10% wametakiwa kurejesha fedha hizo ili zisaidie vikundi vingine.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya maelekezo ya mkopo wa 10% ndani ya halmashauri zote za jiji la Mwanza.

Mhandisi Gabriel amesema kuwa vikundi ambavyo vimehama Mkoa wa Mwanza virejeshe fedha hizo katika halmashauri ambazo zimewapatia ili zisaidie vikundi vingine na kwamba serikali imetoa fedha hizo kwa ajili ya walengwa ambao ni akina mama,vijana na watu wenye ulemavu.

” Ninaomba fedha zirudishwe, tumevipa muda vikundi ambavyo havijatekeleza majukumu ya marejesho ili warejeshe, fedha zote zirudishwe ili ziingie kwenye mzunguko na serikali ione vijana wanakombolewa na kuleta mabadiliko ya kiuchumi ndani ya Mkoa” amesema Mhandisi Gabriel.

Sanjari na hayo amesema kuwa bilioni 1,45,162,500 kati ya zaidi ya shilingi bilioni 5 zilizotolewa kwa vikundi zimerejeshwa katika mfuko wa makundi ya akina mama,vijana na watu wenye ulemavu katika halmashauri za jiji la Mwanza.

Aidha amesema kuwa jumla ya fedha bilion 2,372,690,233.16 zipo tayari  katika halmashauri zote za jiji la Mwanza kwa ajili ya kutolewa kwa vikundi vya vijana, akina mama na watu wenye ulemavu.

Jumla ya shilingi bilioni 4.9 zilizokopehwa kwa vikudi hazijarejeshwa jambo ambalo lilipelekea kukwamisha utaratibu wa kuwakopesha wengine na serikali inajipanga kuchukua hatua za kisheria kwa wahusika kwa mujibu wa sheria ya fedha na serikali ya mitaa sura namba 290  kanuni ya 24

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma