skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. matinde Nestory – Mwanza

Ili kupata tija na kuondokana na uzalishaji duni wa mazao ya kilimo, Wananchi Mkoani Mwanza wameombwa kuendelea kufuata kanuni bora za Kilimo kwa mazao ya chakula na biashara ili kuongeza tija katika uzalishaji.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima wakati wa ufunguzi wa sherehe za wakulima nanenane ambayo ufanyika kila ifikapo Augost 8 kila Mwaka katika viwanja vya Nyamhongolo vilivyopo Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza.

“Nipende kuwashukuru wadau, washiriki na wananchi wa Mkoa wa Mwanza na Mikoa jirani ambayo mmejitokeza kuja kushiriki katika Jambo hili ambalo ni Jambo kubwa tukilitumia vizuri linamstakabali wa muda mrefu katika maendeleo ya sekta ya Kilimo na sekta zingine ambazo zinahusiana na maendeleo ya jamii na maendeleo ya Tanzania kwa ujumla” amesema RC Malima.

Akizungumzia fursa zilizopo katika Kanda ya ziwa ambazo zinachangia katika ukuaji wa sekta ya Kilimo ni  pamoja na uwepo wa ziwa Victoria ambalo  hutumika katika Kilimo Cha umwagiliaji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hasa ukame pamoja na Kanda ya ziwa Magharib ni kituo katika nchi za maziwa makuu pia Mikoa na Kanda za jirani.

Ameongeza kuwa uwepo wa miundombinu ya mawasiliano na usafirishaji pamoja na uwepo wa taasisi za fedha ikiwa pamoja na bank 24 zinazofanya kazi katika Kanda hii.

Aidha amesema kuwa Ziwa Victoria Lina mchango katika sekta ya Kilimo katika kuendeleza uchumi wa uvuvi katika Mkoa wa Mwanza pamoja na serikali imegharamia  mafunzo ya ufugaji wa samaki kwa njia endelevu,visimba na imeainisha maeneo yanayofaa.

“Sekta ya Kilimo, mifugo na uvuvi ndio zinaajiri 63-65% ya nguvu kazi  yote nchini utegemea sekta hizi tatu ambazo uongeza Pato la taifa na Kupunguza umaskini katika Kanda ya ziwa Magharib” amesema RC  Malima.

Kwa upande wake mwenyekiti wa maandalizi ya maonesho ya nanenane Emily Kasagala amesema kuwa Kanda ya ziwa Magharibi inajumuisha Mikoa ya geita, Mwanza na Kagera ambapo ni Mara ya nne kuadhimishwa katika Kanda hiyo.

Aidha katika  maadhimisho hayo ya nanenane ambayo wananchi na Wadau wamepata fursa ya kuona na  kujifunza juu ya bidhaa na huduma zitolewazo katika kubadilishana ujuzi,teknolojia pamoja na mawazo.

Ameongeza  kuwa maonesho hayo ambayo yanajumuisha Wadau mbalimbali  katika kushiriki ikiwemo taasisi za fedha, taasisi za umma,elimu, taasisi za afya, Kampuni za mawasiliano, Kampuni za usambazaji, Kampuni za viywaji,wajasiliamali wa kubwa na wadogo, Kampuni za usambazaji wa pembejeo, Kampuni za zana za Kilimo pamoja na wakala wa serikali.

Katika maonesho hayo Wadau hupata fursa ya kuonesha shughuli zinazohusiana na Kilimo,mifugo,uvuvi, ikiwa ni pamoja na  shughuli za umwagiliaji, utafiti,hifadhi ya mazao,usindikaji wa mazao, matumizi ya pembejeo na zana za Kilimo

Akizungumzia changamoto amesema kuwa ukosefu wa miundombinu ya kudumu hali ambayo inasababisha kuongezeka kwa gharama za uratibu wa maonesho.

Nae mmoja wa washiriki katika maonesho hayo Fidel Michael ambaye ni  meneja mahusiano wa biashara za Kilimo bank ya NMB amesema kuwa Wadau wa mifugo,Kilimo na uvuvi  wameongeza thamani ya mazao ya Kilimo kwa kuwapa mikopo ya mitaji kwa ajili ya uwekezaji kwa riba  nafuu 9%.

Sambamba na hayo amewataka wakulima kuchangamkia fursa za kibenk katika kuendeleza Kilimo chenye tija na kujipatia kipato.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma