Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Na. Kadislausi Simon – Kigoma
WAKULIMA Katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma, Wameiomba Serikali kuongeza Mabwana Shamba na Maafisa Ughani Ngazi ya Vijiji na Kata, Ili Kusaidia Shughuli za Kilimo kuwa na Tija kwa Wakulima na Kuachana na Kilimo Mazoea ambacho wakulima Wengi wamekuwa wakipata hasara kubwa ya kukosa Mazao.
Wamesema hayo wakati wa Mafunzo ya Mradi wa Kuboresha Sekta ya Kilimo ulioandalia na Shirika la TAWEA na kwamba Msimu wa Masika Umewadia na Rafiki wa Mkulima Ni Jembe,Ambapo uhitaji wao ni kuona wanawezeshwa Pembejeo kwa wakati na elimu ya kukabiliana na magonjwa yanayoharibu mazao.
Uhitaji huo unalifanya shirika la TAWEA ambalo linakuja na mpango wa kuboresha Sekta ya kilimo ukianza na kata tano za Wilaya ya Kigoma ambapo wataalamu wa masuala ya Kilimo akiwemo afisa Kilimo Halmashauri ya wilaya ya Kigoma James Pitter wanaeleza manufaa kupitia mradi huo ikiwemo kuwaunganisha wakulima kwa pamoja.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi Shirika la TAWEA Festo Mlina amesema wameamua Kuungana na serikali na kuja na mpango wa ufuatiliaji masuaal ya Kilimo kwa lengo la kuweka ushirikishwaji wa wakulima na maafisa ughani na kuleta tija katika sekta ya kilimo.