skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Profesa Joyce Ndalichako aingilia kati malalamiko yao, aagiza mamlaka za udhibiti kuchukua hatua

Siku mbili tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu Samia Suluhu Hassan akiri kuwepo kwa changamoto za usambazaji na uuzaji wa mbolea ya ruzuku na kuagiza wizara ya kilimo kuchukua hatua za haraka kutatua kero za mawakala, zaidi ya wakulima 200 kutoka wilaya za Kasulu na Buhigwe wamekwama mjini Kasulu baada ya mawakala kushindwa kuwauzia mbolea.

Tukio hilo limetokea jana Jumatano ambapo wakulima hao walilazimika kuandamana Kwenda kumlalamikia Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini Profesa Joyce Ndalichako ambaye alilazimika kusitisha safari yake ya kwenda Dodoma na kuwasikiliza wakulima hao.

Katika madai yao wakulima wamelalamikia kuwepo kwa vitendo vya upendeleo na rushwa sambamba na mfumo unaotumika kusajili na kuhakiki wakulima kutengemea mitandao ya internet ambayo haina ubora na uhakika wa mtandao.

George Wilison Maguge kutoka Kijiji cha Kabulanzwiri amebainisha kuwa wakulima wengi wamekaa mjini kwa Zaidi ya siku tatu bila kuuziwa mbolewa hukuu mawakala wakiwauzia walanguzi na kuwaacha wananchi huku wakijibiwa majibu ya kudharauliwa wakiwambiwa kuwa hakuna mbolea ilihali wakiiona ndani ya maghala

“Wanatuambia kuwa hakuna mbolea, mara hakuna stika za mbolea ya ruzuku, wakipigiwa kelele wanaambiwa kuwa stika zilizopo ni za mbolea za kukuzia wakati huu ni msimu wa kupanda, hii ni dharau kwa viongozi wa serikali, wanawadharaulisha na kusababisha serikali ichukiwe, viongozi wa wilaya wamehongwa na hawatetei wakulima, nashauri wachunguzwe. Alisisitiza Bw. George Wilson

Profesa Ndalichako (katikati) akizungumza na wakulima baada ya kupokea malalamiko yao ya kukosa mbolea kwa mawakala mjini Kasulu

Mfumo wa utoaji wa mbolea ya ruzuku kwa njia ya namba za usajili na stika maalumu kwa kila mkulima umekuwa na tija pamoja na athari kadhaa ikiwemo wanawake kushindwa kuhudumiwa na mawakala,, kulala mazingira hatarishi wakisubiri mawakala huku pesa zao zikiwa hatarini kuporwa na vibaka.

“Sisi wanawake tunateseka sana, tuna siku mbilii tumekuja kununua mbolea tunalala nje na Watoto wetu baridi na mvua, na kuna matishio ya vibaka kujaribu kuporwa pesa zetu, yote haya yanafanyika wakati mawakala wana mbolea ghalani na hawataki kutuuzia wanasema mtandao mbovu kwenye mfumo, lakini wanawauzia wengine pembeni huku tukishuhudia, tunaomba Waziri Ndalichako kama ulivyomwambia Rais wetu hadharani, rudi kamwambie tunanyanyaswa” Alisisitiza Bibi Renatha Kahandwa kutoka Kijiji cha Mnyegela wilaya ya Buhigwe.

Mlalamiko hayo yanaunga mkoano na Bibi Happiness Rugina kutoka Kijiji cha Ruhita ambaye alinusurika kuporwa fedha na vibaka majira ya saa 10 alfajirii akiwahi kupanga mstari kwa wakala ambapoo hata hivyo aliambiwa kuwa mbolea haipo huku akiishuhudia ikiuzwa kwa wenye pesa nyingi kwa bei ya juu tofauti na maelekezoo ya Rais Samia.

Kufuatila malalamiko hayo Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, vijana na wenye Ulemavu profesa Joyce Ndalichako ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini, amelazimika kufanya ziara ya kushtukiza kwa mawakala wa kampuni za YALLA na ETG ambapo amehuhudia mamia ya wakulima wakiwa wamekwama kupata mbolea ya ruzuku

Profesa Ndalichako amehoji sababu za wakilima kusumbuliwa na kujibiwa na Bw. Sebastian Mganya ambaye ni wakala mkuu wa kampuni ya Yalla akidaii kuwa kinachosababisha kuzorota kwa uuzaji wa mbolea ya Ruzuku ni mfumo wa matumizii ya data mtandao ambao hauna ubora pamoja na kukosekana kwa stika ambazo ni lazima zipandikwe na kuskaniwa na mfumo huo kabla ya mkulima kupata mbolea yake.

Aidha Bw. Mganya ameulalamikia mfumo huo akidai kuwa endapo hautatafutiwa ufumbuzi wakulima watapata shida Zaidi kwakuwa hakuna wakala atakayekubali kupata hasara kupitia mfumo huo ambaoo unachelewesha utoaji na uuzaji wa mbolea huku msimu wa kupanda ukiyoyoma, na kuiomba serikali kutoa bei elekezi sambamba na madaftari ya usajili na uhakiki kwa mawakala ili wanapouza wawaandikishe wakulima katika madaftari hayo badaya ya kuutegemea mtandao wa internet ambao siyo wa uhakika.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea kanda ya Kati Bw. Joshua Ng’ondya amewaomba radhi wakulima pamoja na mbunge wa Kasulu Profesa Ndalichako kutokana na usumbufu wa kuchelewa kufika kwa mbolea pamoja na stika na kuahidi kuwa atasimamia utatuzi wa changamoto zote ndani ya masaa 24, huku akieleza kuwa stika za kutosha zitawasili na ndege ya Alhamisii kutoka Dar es salaam

Bw. Ng’ondya amekiri kuwa kumekuwepo na kusuasua kwa mfumo wa usajiri, uhakiki na uuzaji wa mbolea kwa njia ya mtandao na kubainisha kuwa wataalamu kutoka wizara ya kilimo pamoja na mamlaka ya udhibiti wanaendelea kufanyia kazi na kutatua changamoto mbalimbali za imfumo, na kwamba shehena kubwa Zaidi ya mbolea itawasili mkoani Kigoma siku ya alhamisi (leo) na kusambazwa kwa mawakala mbalimbali katika wilaya zote za mkoa wa Kigoma.

Kuhusu vitendo vya Rushwa kwa watumishi wa kada ya ughani na maafisa wanaosajili wakulima kwenye mfumo, Bw. Ng’ondya ameeleza kuwa zoezii la usajili ni endelevu hadi Desemba mwaka huu na kwamba mkulima hatakiwi kutoa pesa kwa ajili ya usajili, huku akitoa namba za simu ili mkulima atakayeombwa pesa atoe taarifa ili hatua zichukuliwe haraka.

Kwa upande wake Waziri ofisi ya Waziri mkuu, Kazi, afira, vijana na wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako alitoa onyo kali kwa mawakala wote pamoja na watumishi wa idala ya kilimo akiwataka kutimiza wajibu wako kwa mujibu wa sheria na maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

“Mnataka kumchafulia Rais kazi yake nzuri iingie do ana kumchonganisha na wanachi, yeye ametoa ruzuku ili kupunguza ukali wa bei kwa wakulima harafu nyinyi mnamhujumu kwa kutowahudumia wananchi wake, mimi sitakubali jambo hili liendelee, hakikisheni mfumo unafanya kazi, hakikisheni stika zinapatikana na pia ongezeni vituo vya mauzo katika kata mbalimbali ili wananchi waepuke usumbufu kama huu ambao ni hatari kwa usalama wao.” Ameonya Waziri Ndalichako na mbunge wa Kasulu mjini.

Aidha Profesa Ndalichako aliwasilisna na mbunge wa Nzega mjini Bw. Husein Bashe ambaye ni Waziri wa Kilimo naye akaonesha kusikitishwa na wakilima kusumbuliwa na kuahidi kulifanyia kazii haraka.

“sitamfumbia macho yeyote anayekwamisha juhudii za Rais hapa Kasulu n ahata katika majimbo mengine ndani ya mkoa wa Kigoma, nitawafuatilia na nitajulisha mamlaka ya Rais kuhusu uhujumu au uzembe wowote nitakaoubaini, ninafuatilia suala hili usiku kucha, kwaniyo tusionane wabaya, Meneja wa TFRA timiza wajibu wako, simamia ongezeko la mawakala tuhuwahudumie wakulima, vingine tafuta kazi nyingine ya kufanya katika hili sitakuvumilia. Alisisitiza Ndalichako kwa machungu.

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi katika viwanja vya Kiganamo mjini Kasulu juzi, alikiri kuwa kumekuwepo na uchache wa mawakala wa mbolea ya ruzuku na kuwaahidi wananchi kuwa atamwagiza Waziri Bashe kutatua changamato zote za upatikanaji, usambazaji na uuzaji wa pembejeo ikiwemo mbolea iliyowekewa Ruzuku na serikali.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma