skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Tanzania imeanza utoaji wa chanjo kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi wanaoishi katika kambi magaribi mwa Tanzania.

Tanzania ina wakimbizi Zaidi ya 200,000 wanaohifadhiwa katika kambi tatu za Nyarugusu, Mtendeli na Nduta mkoani Kigoma,  na Uzinduzi huo umefanyika katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu ambapo wakimbizi Zaidi ya 20 wamechanjwa katika hatua ya awali baada ya elimu kutolewa na viongozi wa serikali, mashirika ya umoja wa mataifa yanayohudumia wakimbizi pamoja na viongozi wa dini katika mkutano wa hadhara ambao hata hivyo mahudhurio yake yalikuwa hafifu

Akiongea baada ya kuchanjwa, Bw. Nyange Eninga mkimbizi kutoka DRC amesema yeye ameamua kuwa mfano wa kuigwa na kwamba amehamasishwa na historia ya uwepo wa chanjo nyingine

Hata hivyo wengi wa wakimbizi wamekuwa na mashaka juu ya chanjo hiyo licha ya elimu inayotolewa kutokana na kile wanachotaja kuwa hawajashuhudia maambukizi yoyote ya corona kambini humo. Dina londa ni mmoja wa wakimbizi waliotoa maoni ya mashaka juu ya chanjo hiyo

Kihutubia katika hafla ya uzinduzi wa utoaji chanjo Mkuu wa kambi hiyo kutoka wizara ya mambo ya ndani Bw. Siasa manjenje licha ya kutangaza kuwa yeye mwenyewe amechanja, amewatoa hofu wakimbizi kuhusu usalama wake.

Ripoti ya Prosper Kwigize, mwandishi wa kimataifa alipozuru kambi ya Nyarugusu

Mkuu wa UNHCR Kasulu Bw. Ben Boubacar Diallo ametoa wito kwa wakimbizi kuipokea Chanjo kama moja ya huduma mhimu kwao kutoka kwa wahisani pamoja na serikali.

Imeelezwa kuwa licha ya kuwepo kwa taarifa zisizosahihi kuhusu chanjo dhidi ya COVID-19 mkoa wa Kigoma umefanikiwa kutoa chanjo kwa watu Zaidi ya 30 elfu na kwamba mwitikioo ni mkubwa. Hayo yamethibitishwa na kaimu mganga mkuu wa mkuu wa mkoa Kigoma Dr. Hoseam Willium

Takribani dozi 50 elfu zimetengwa kwa ajili ya wakimbizi katika kambi zote ili kuwakinga dhidi ya COVID 19

Ifuatayo ni sauti ya mwandishi wetu ambaye pia ni mkurugenzi wa Buha Radio alipotembelea kambi ya Nyarugusu kushuhudia uzinduzi wa Chanjo ya UVIKO 19 kwa wakimbizi. Bofya usikilize

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma