skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Adella Madyane, Kigoma

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limewakamata watu tisa wanaotuhumiwa kujihusisha na usafirishaji na uuzaji wa viungo vinavyodhaniwa kuwa ni viungo vya miilii ya binadamu ambavyo vinahisiwa kuwa vinatumika katika shughuli za kishirikiana na uchawi

Akiongea na waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, ACP James Manyama amesema, watu hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki katika Kijiji cha Kanyonza wilayani Kakonko mkoani Kigoma katika kuzuizi cha polisi Kihomoka barabara kuu iendayo mkoani Kagera ambapo ukaguzi hufanyika kwa abiria na mizigo.

Baadhi ya vifurushi na mizigo yenye madawa ya kienyeji ambamo viungo vya binadamu vilikutwa. Picha na Adella Madyane.

Kamanda Manyama alibainisha kuwa awali watu watatu  walikamatwa katika kuzuizi hicho cha polisi wakiwa kwenye gari yenye namba za usajili T 948 DQU aina ya Pro Box (mchomoko) wakielekea Mwanza kwenye kijiji cha Nyahunge ambako ambapo inadaiwa kuwa walikuwa wakipeleka viungo hivyo kwa mtu aliyekuwa amewaagiza.

Inaelezwa kuwa baada ya kuwahoji watuhumiwa waliwataja wateja wao ambao ni wakaji wa jijini Mwanza ambao pia ni wenyeji wa mkoa wa Kigoma na pia kuwataja watu waliowezesha upatikanaji wa viungo hivyo ambao walibainika kuwa ni wakazi wa wilaya ya Buhigwe.

Jeshi la polisi mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani Mwanza tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine sita waliohusika kwenye tukio hilo na walikiri kwamba viungo hivyo walivifukua kutoka kwenye kaburi la mtu anayedhaniwa kufariki Mei 1, 2022 katika kijiji cha Migongo kilichopo wilayani Buhigwe mkoani Kigoma” alibainisha RPC Kigoma

Viungo vilivyobainika katika ukamataji huo ni sehemuu ya mbavu na mguu wa binadamu, jambo linalotia hofuu juu ya uwepo wa biashara hiyo ya uuwaji na ukataji wa viungo au ufukuaji wa makaburii mkoani Kigoma na maeneo ya jirani.

Kutokana na sakata hilo jeshii la polisii linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuubaini mtandao mzima wa mauaji, ukataji wa viungo na uhalifuu mwinginie katika mkoa huoo wa pembezoni mwa Tanzania eneo la magharibi

Mkoa wa Kigoma umekuwa ukitajwa kuwa miongoni mwa miko yenye matukio mengi ya uhalifu na mauaji na ni miongoni mwa mikoa iliyokumbwa na kadhia ya mauaji ya watu wenye ualbino na ukataji wa viungo katik aya mwaka 2007/2010.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma