skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Simiyu

Mawakala wote wa uuzaji na usambazaji wa gesi mkoani Simiyu wamepewa wiki moja kuhakikisha wanaanza kutumia mizani ambayo imehakikiwa na wakala wa vipimo na kuanza mara moja kupima ujazo wa gesi kabla ya kuwauzia wateja wao.

Hayo yamesemwa na kaimu meneja wa wakala wa vipimo mkoani Simiyu Tuntufye Mkumbwa wakati wa kikao kilichohusisha mawakala wakubwa na wadogo wa gesi mkoani humo kilichofanyika mjini Bariadi, ambapo amewataka wale wote wasiotumia mizani kwa ajili wa kupima gesi kabla ya kuiuza waanze mara moja.

“Wauzaji wote wa gesi wanapaswa wawe na mizani iliyohakikiwa na wakala wa vipimo na nitoe agizo  ndani ya wiki moja  kila muuzaji wa gesi anatakiwa kuwa na mzani na kwa upande wa ufungashaji wa gesi, mitungi yote ambayo haitakuwa na uzito wa mtungi pekee yake nawapa miezi mitatu ili waweze kurekebisha mitungi yao wakishindwa kufanya hivyo tutakapopita kwenye ukaguzi tukiwakamata watalipa faini ambayo haipungui kuanzia laki moja mpaka milioni ishirini.” amesema Mkumbwa.  

Bw. Tuntufye Mkumbwa kaimu meneja wa wakala wa vipimo mkoani Simiyu

Emmanuel Julius ni wakala mkubwa wa usambazaji wa gesi mkoani Simiyu amesema  matumizi ya mizani yatawasaidia wateja kuhakikisha gesi wanayonunua inakuwa na ujazo ulio sahihi na unaotakiwa.

“Kutumia mizani inakuwa inawasaidia wateja wetu (mawakal wadogo) kuhakikisha gesi ambazo zinatoka kwetu zinakuwa na ujazo ulio sahihi kwenda kwa mteja wa mwisho, pia changamoto wanazokutana nazo mawakala wetu unakuta wamepokea zile gesi na hawajui zile namba za mitungi kwamba zinahusiana na nini ndio hizo ambazo tunawasaidia kuwaelimisha, unakuta kuna namba mbili kuna 30.5 halafu kuna 15.5 sasa unakuta yule mtumiaji wa mwisho hajui zile namba zina maana gani, tunawaelimisha kwamba hii 30.5 ni ujazo wa gesi pamoja na tupu lake.” amesema Julius.

 Nao mawakala wadogo wa gesi wamesema kikao hicho kimewakumbusha mambo mengi  sambamba na  utatuzi wa changamoto  uwepo wa changamoto n huku mmoja wa watumiaji wa gesi akisema  ujio wa gesi ni mkombozi wa mazingira ambapo  ameongeza kuwa kuna wakati akinunua gesi haitumiki muda mrefu na awali hakujua kama kuna umuhimu wa kupima gesi kabla ya kuondoka eneo aliliuziwa gesi hiyo.

“Kikao hiki kimenipa elimu ambayo itanisaidia kwa wateja wangu kimenipa kujiamini katika  biashara yangu ya gesi hasa pale  ninapokutana na changamoto kutoka kwa wateja wangu,kwamba labda mbona gesi  hii inaonekana haijajaa basi imenielimisha mimi zaidi  kuweza kujua ni vizuri  nikafatilia ujazo wa gesi, uchakavu wa mitungi ili niweze kufanya biashara hii kwa umakini zaidi na nitafanya biashara yangu kwa uhakika na kujiamini ili mteja wangu wa mwisho atakuwaakiamini huduma hii ina ubora zaidi” amesema Adelina Matemu, wakala mdogo wa gesi .

“nimejikumbusha namna ya ujazo wa mtungi, unakuwa umeandikwa ujazo wa gesi  iliyopo na uzito wa mtungi  kwa hiyo tutaweza kuwaelimisha wateja wetu (watumiaji) ,changamtoto zipo japo sio nyingi mfano mtungi kupungukiwa gesi tunawasiliana wa wakala wakuu wanabadili mitingi yenye changamoto na kutupa mingine , tumekuwa tukiwasiliana na mawakala wakubwa na utatuzi unakuwepo na kuhusu suala la mizani tumelipokea , linanitoa wasiwasi kati yangu mimi na mnunuzi  wa mwisho naona pale patakuwa hakuna ulalamishi zaidi kwasababu kuna mtu anaweza kuchukua bila kupima na akienda kwake anarudi anasema gesi ilikuwa nusu lakini tukiweka mzani na akapima basi  kila mtu ataridhika” itatusaidia kuepuka malalamiko”amesema Kitenge Hamis, wakala mdogo

Ester Joseph ni mtumiaji wa gesi amesema ujio wa gesi ni mkombozi wa mazingira huku akiongeza kuwa kuna wakati akinunua gesi haitumiki muda mrefu na awali hakujua kama kuna umuhimu wa kupima gesi kabla ya kuondoka eneo aliliuziwa gesi hiyo.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma