skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory

Wafanyabiashara takribani 650 wa soko la Kirumba lilipo jijini Mwanza wametakiwa kuondoa hofu juu ya Kupata wateja wanapohamia kwenye uwanja wa magomeni ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa la kirumba.

Rai hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya kirumba Wessa Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya ujenzi wa soko la kirumba.

Amesema kuwa kila mfanyabiashara atatengewa eneo lake Kutokana na biashara anayofanya pindi soko la kirumba litakapokamilika.Diwani Juma amesema kuwa uwanja wa magomeni wameshapeleka huduma za choo matundu 6,maji pamoja na umeme ambapo wakati wowote wanahamia wafanyabiashara.

Diwani wa kata ya kirumba Wessa Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake

“World bank imetoa bilioni17 kwa ajili kujenga soko la kisasa la kirumba la ghorofa moja pamoja na barabara za kilometers 2.9 zinazozunguka soko hilo jipya hivyo kila mfanyabiashara ambaye amejiandikisha na kupigwa picha hatapoteza nafasi yake na hata majengo yale mnayojenga magomeni ni kwa gharama zenu Soko la kirumba likimalizika mtavunja wenyewe na uwanja utaendelea kutumika Kama hapo awali”amesema Diwani Juma.

Kwa upande wake mwenyekiti wa soko la kirumba Elias Daud amesema kuwa wafanyabiashara wameanza kupewa maeneo na kujiandaa kuhama sokoni hapo ili kupisha ujenzi wa soko jipya la kirumba.

“Wafanyabiashara wanatakiwa kuondoa hofu kuhusu wateja sababu wateja wanaonunua kirumba ndio hao hao watakaokuja kununua magomeni maana tunahama na biashara Zetu na tunahama wote kwa pamoja”amesema Daud.

Sanjari na hayo amesema kuwa serikali imesaidia kujenga soko la kirumba ambalo muda mrefu mazingira, ubora na miundombinu yamekuwa sio rafiki.

“Choo,maji,na umeme tayari uwanja wa magomeni,mitaro ni changamoto Kuna maji ambayo yanakatiza uwanjani hivyo tunaomba serikali kuangalia ujenzi wa mitaro kidogo tunaweza kujichanga tukatengeneza wenywe ili kuondoa maji yanayozalishwa ndani ya soko lakini mitaro mikubwa serikali utusaidie kujenga ili kuja kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza kipindi Cha Mvua  Kutokana na maporomoko ya maji”amesema mwenyekiti Daud.

Hata hivyo ujenzi huo wa soko hilo ambao unatarajiwa kuchukua takribani Mwaka mmoja na miez sita mpaka miaka miwili kukamilika kwa soko la kisasa.

Nao baadhi ya wafanyabiashara wamesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kujenga soko la kisasa hali ambayo itasaidia kuwa katika hali ya usalama pamoja na Kupata wateja kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza na Mikoa jirani.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma