skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Wadau wa maendeleo kutoka wilaya ya Kasulu, wametembelea na kupata maelezoo kuhusu kituoo cha uzalishaji wa maudhui cha BUHA FM Radio cha Mjini Kasulu mkoani Kigoma ambacho kinatarajia kuanza shughuli zake mwaka huu baada ya kukamilisha taratibu za leseni.

Fundi Mitambo Mr. George akitesti mitambo ya BUHA STUDIO

Miongoni mwa waliotembelea studio zetu ni Abeid Kapori ambaye ni mkurugenzi wa Shirika la PATA linalojishughulisha na masuala ya utetezi wa haki za watoto na utawala bora na pia Makamu mwenyekiti wa mtandao wa Jamii wa mawasiliano ya kidigitali KACONECOS

Studio za Buha FM zinazoendelea kujengwa zitatumika kuzalisha vipindi vya kijamii pamoja na habari shirikishi zinazokidhi ubora kwa kiwango vya kimataifa na kwa kuzingatia maadili na kanuni za utangazaji kwa mujibu wa sheria za EPOCA

Buha FM Radio inaasisiwa na shirika la Uwekezaji na maendeleo (OHIDE) lenye makao makuu wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma