skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Wilaya ya Kasulu ni miongoni mwa wilaya kongwe nchini Tanzania, ni wilaya yenye mgawanyo wa utawala katika halmashauri mbili za Kasulu mjini na Kasulu vijijini, ina idadi kubwa ya watu wanaokadiriwa kufikia watu laki sita wakiwemo wakimbizi kutoka nchi za jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pamoja na Jamhuri ya Burundi.

Kasulu ni wilaya yenye watu wachapa kazi hasa katika Kilimo na biashara, kuna hifadhi na pori la akiba la Moyowosi na mto mkubwa wa Malagarasi unaochangia maji katika ziwa Tanganyika, Kasulu inapakana na nchi ya Burundi na ina ardhi oevuu inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali.

Muonekano wa Mji wa Kasulu mkoani Kigoma ambao una kiu ya kuwa na kituo cha Radio

Pamoja na ukubwa na umaarufu wa wilaya ya Kasulu inayoubeba mkoa wa Kigoma kiuchumi, wilaya hiyo kongwe haina kituo cha Radio kinachorusha mawimbi yake kutokea wilayani humo. Hali hii inapelea jamii ya Kasulu kuwa wasikilizaji tu badala ya kutoa mchango wao katika mijadala na habari mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni

Kuanzishwa kwa kituo cha Buha FM,, kumeibua hisia za shangwe na furaha kwa makundi mbalimbalii ya kijamii hususani vijana, wanawake na wazee ambao wanaamini kuwa sasa jukwaa limepatikana na kwamba watapaza sauti zao ili kuharakisha maendeleo.

Mchungaji Gervas Baragomwa wa Kanisa la Christian Gospel Church of Tanzania la mjini Kasulu

Miongoni mwa wanaodhihirisha furaha zao ni viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali, wakiwemo mashekhe, mapadre, wachungaji na watawa ambao kwa nyakati tofauti wametembelea kituo cha Buha FM na kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo kuongoza sara za baraka.

Shekhe Masoud Kikoba – Shekhe mkuu wa wilaya ya Kasulu alipozuru Buha FM hivi Karibuni

Shekhe Masoud Kikoba, Mchungaji Gervas Baragomwa, Bruda Valentine Buberwa ni miongoni mwa waliotembelea Radio hiyo na kupongeza juhudi za shirika la OHIDE kwa kubuni na kuanzisha Radio hiyo

Sikiliza maombii ya mchungaji Baragomwa aliyotoa hivi karibuni kwa kubonyeza kutufe hapa chini.

Buha FM inawakaribisha wananchi kuja kushuhudia kituo chao na kutoa maoni

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma