skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory, Mwanza

Wahitimu wa vyuo na vyuo vikuu mkoani mwanza wametakiwa kutumia talaama na ujuzi walioupata vyuoni katika kuiletea maendeleo jamii pamoja na kuijenga nchi.

Rai hiyo imetolewa June 12 mwaka huu na Katibu  wa uchumi na fedha ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu CCM Dr Frank Hawasi katika mahafali ya kumi (10) ya wahitimu wa vyuo na vyuo vikuu ambao ni makada wa Chama cha mapinduzi( CCM) yaliyofanyika katika ukumbi wa bank Kuu jijini Mwanza

Mahafali hayo ya vijana wa CCM  yalijumuisha wahitimu mia tano (500) kutoka vyuo vya MIPANGO, FISHERIES, CBE, TIA, DIT na IFM vilivyopo katika jiji la Mwanza, ambapo pamoja na wito wa kutumia taaluma yaoo vizuri wamehimizwa kuwa wazalendoo na mfano wa kuigwa katika jamii.

Dr Hawasi alisema  kuwa wahitimu wanapaswa kutumia elimu waliyoipata vyuoni Katika  kuleta maendeleo ya nchi na kuweza kufikia malengo na ushirikiano pamoja na kutekeleza ahadi ya chama na wanachama kwa ujumla.

Ni kosa kupata utalaam halafu unakaa nao bila kuupeleka kwa jamii Taifa ambalo watu wake hawapendi kujifunza watabaki nyuma Katika kuleta maendeleo kwa jamii” amesema Dr Hawasi.

Kutoka kushoto Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi wa pili kushoto mwenyekiti wa Senet Christian Kumari katikati Dr Frank Hawasi katibu wa uchumi na fedha na wa pili kulia ni katibu wa CCM Mkoa comred Julius Peter

Aliongeza kuwa vijana wamepaswa kutumia weledi na maarifa pamoja na taaluma waliyoipata chuoni ambayo itasaidia kujikwamua kiuchumi. 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nyamagana  Amina Makilagi ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa wahitimu ni vyema kuacha anwani ambazo zitawasaidia kupatikana na kuwapatia ajira pamoja na kufanya kazi kwa bidii katika kuliletea maendeleo taifa.

Nyie ni zao la CCM hakikisheni mnaacha anwani za makazi ya kudumu ili pale mtakapohitajika tuwapate kwa urahisi “amesema  DC Makilagi

Akisoma risala katibu  Senet Idara ya vyuo na vyuo vikuu  Salim Selestine alisema kuwa Seneti Mkoani Mwanza wamefanikiwa kuongeza wanachama kutoka 1400 hadi kufikia 2000 ingawa idadi hiyo huongezeka na kupungua kutokana na udahili wa wahitimu wa wanachuo vyuoni.

Alibainisha kuwa mbali na kuwa na mafaniko bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili hususani ukosefu wa pesa jambo ambalo husababisha kujiendesha kwa michango binafsi.

Fedha tunazozipata kutoka kwa wazazi,  walezi na wafadhili ndio tunatumia na wakati mwingine hata hiyo michango haifikii malengo hiyo kupelekea kushindwa kufanya semina za mafunzo ya kiuongozi na utendaji kwa viongozi wa matawi ili waweze kujua majukumu yao na kufahamu mipaka ya kiutendaji” Amesema Selestine.

Alifafamua kuwa ukosefu wa kadi za vijana hupelekea kuwa na kundi kubwa la vijana ambalo kwa namna moja ama nyingine wakiingia vyuoni ndio wanakutana na mambo ya kisiasa na  kuwiwa kujiunga na chama hicho.

” Ukosefu wa kadi umepelekea kuwa na wanachama wa maneno na kushindwa kuwasajili ndani ya jumuiya kwani hakuna kadi za kuwapa pindi wanapohitaji” Amesema Selestine.

Aidha amesema kuwa mbali na changamoto hizo chama kinapaswa kutoa kadi 300 kwani itasaidia kuongeza wanachama kwenye jumuiya pamoja na kuongeza kipato ambacho kitawasaidia kupata ruzuku ya kuendesha shughuli za senet.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma