Na. Irene Bwire -PMO na Anita Balingilaki Buha - Simiyu WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka…
Vijana Zaidi ya elfu ishirin na sita wa chama Cha mapinduzi Mkoa wa Mwanza wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika chama hicho.
Taarifa hiyo imetolewa Leo na katibu (UVVCM) Mkoa wa Mwanza Denis Nyamlekela Kankono wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho na kusema kuwa vijana wamejitokeza katika kuwania nafasi mbalimbali katika chama hicho ambapo uchanguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 19 mwaka huu katika ngazi za jumuiya zote katika Mkoa wa Mwanza.
“Nikiwa Kama Mkurugenzi wa uchaguzi nimejipanga na kuhakikisha wagombea ni wenye sifa hakuna upenyo watu wenye sifa ndio wamepata nafasi ya kugombea na kwa yeyote mgombea atakayebainika Kuna vitendo vyovyote vya rushwa atakamatwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU ambayo ipo na itawachukulia hatua za kisheria.”amesema katibu Kankono
Akielezea nafasi zinazogombewa ni pamoja na nafasi ya Mwenyekiti,katibu, wajumbe wa mkutano mkuu kata,wajumbe wa mkutano mkuu wilaya na wajumbe wa baraza kata na nafasi zote Zina mgombea zaidi ya mmoja.
Katibu UVVCM Kankono ameeleza kuwa uchaguzi huo utakuwa wa amani na haki na kuhakikisha wagombea wameridhika na matokeo ya uchaguzi .
Aidha amewataka wagombea watakaochaguliwa watende haki kwa kubuni miradi katika maeneo yao hali ambayo itasaidia kuinua uchumi wa Tanzania.
Hata hivyo amewataka wagombea ambao kura zao hazitatosha wawe na utulivu na kuondoa chuki pindi uchaguzi utakapokuwa umekwisha na kushirikiana na wale walioshinda katika uchaguzi huo katika kukijenga chama Cha mapinduzi na kuwa Imara.