skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Matinde Nestory, Mwanza

Vijana nchini wamehimizwa kujiunga katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali ikiwemo ufugaji wa Samaki katika mfumo wa Vizimba ziwani pamoja na kufanya kazi kwa bidi na uadilifu ili kujipatia kipato na kuepuka umasikini

Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Mifugo na uvuvi Abdalah Khamis ulega wakati wa hafla ya wahitimu mafunzo ya ufugaji samaki kwa njia ya vizimba kutoka mkoa mzima wa Mwanza iliyofanyika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Naibu waziri Ulega amesema kuwa vijana wanatakiwa kuwa wadilifu na makini katika ufugaji samaki ambao utaleta matokeo mazuri katika sekta ya uvuvi na kutengeneza ajira kwa vijana na kuongeza Pato la taifa.

“Ni lazima  waendeleze ajenda ya uzalishaji kwa kuwatazama na kuweka mfumo na mtandao nzuri wa masoko sio tuzalishe Kisha hatujui tunapeleka Wap tutashirikisha viwanda vinavyochakata minofu ya samaki na wengine kuifungua masoko makubwa” amesema Naibu wazir Ulega.

Baadhi ya vijana walioshiriki mafunzoo ya ufugaji wa samaki kwa njia ya Vizimba katika ziwa Victoria

Aidha Mheshimiwa Ulega ameitaka Bank ya Kilimo kutazama bilioni 20 alizotoa Rais Samia kwa ajili ya Vijana na makundi mengine ya Ushirika kupata fedha hizo.

Kwa upande wake katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Emil Kasagara amesema kuwa vijana hao waliohitimu mafunzo ya ufugaji samaki kwa njia ya vizimba ndani ya ziwa Victoria kutoka katika halmashauri ya jiji la Mwanza, Ilemela, Magu pamoja na Misungwi.

Ameongeza kuwa eneo la ziwa Victoria upande wa Tanzania kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Mara,Kagera na Simiyu  ambapo Mkoa wa Mwanza una miliki 48% sawa ni kilometers 16842.

Amesema kuwa lengo la kuanzisha mradi huo ni pamoja na Kupunguza tatizo la ajira kwa vijana,mradi ulilenga kuongeza uzalishaji wa samaki ndani ya ziwa Victoria pamoja na kuongeza kipato kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza.

Nae Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa uvuvi Tanzania (TAFIRI) Baraka Sekadende amesema kuwa wamefanya utafiti katika maeneo yanayofaa kufuga samaki kwa njia ya Vizimba ambapo lengo likiwa kupunguza gharama za mwekezaji Kupata maeneo hayo pamoja na Kupunguza mlolongo wa upatikanaji wa vibari kwa ajili ya ufugaji samaki kwa njia ya vizimba.

“Mikoa ilipokea barua katika halmashauri husika ambazo zilikuwa ni halmashauri za Mkoa wa Mwanza na halmashauri za Mkoa wa Kagera baada ya hapo waliainisha maeneo kwa vigezo waliopewa kwenye barua na wakatuletea maeneo ambayo walipendelea ili tuwafanyie utafiti tumefanya utafiti katika mikoa hiyo miwili na katika Mkoa wa Mwanza tumefanya utafiti katika halmashauri ya Ilemela, Nyamagana, Sengerema, Buchosa, Misungwi, Magu na Ukerewe” amesema Sekadende.

Amebainisha kuwa jumla ya maeneo ambayo wamefanya utafiti yalikuwa 36 kwa Mkoa wa Mwanza na Kagera  Maeneo yaliyofaa ni 23 ambapo wameangalia kina Cha sehemu husika kisiwe chini ya mita tano kwenda chini.

Akizungumzia vigezo amesema kuwa wamefanya utafiti kwa kuangalia kiwango Cha oxygen kilichopo katika eneo hilo,kiwango Cha PH,Virutubishi vinavyopatikana eneo hilo  pamoja na vimelea ambavyo samaki wanakula.

Kwa upande wake Mbunge wa vijana Mwasi Kamani amesema kuwa Mkoa wa Mwanza unamiliki 51% eneo lote la ziwa Victoria ambapo tumesajiri vikundi 64 ambavyo vina wanachama 320 akina mama,vijana na watu wenye ulemavu na  vikundi 10 wameombewa kiasi Cha  fedha bilioni 2.5  kwa ajili ya Vizimba 58 ambayo mpaka sasa imeshapita takribani  miezi mitano.

Akizungumzia changamoto amesema kuwa urasimu katika taasisi ambazo zinatoa vibari,urasimu katika bank ya Kilimo (TIDB), vijana hawana sifa za kukupesheka pamoja na Vijana kukata tamaa kwa kucheleweshewa fedha hizo.

“Tunakuomba Rais Samia atuangalie vijana kupitia bank hii ya Kilimo ili tuweze kukopeshwa pia tujengewe uwezo wa Kupata fedha ili tufanye kazi”amesema Mbunge Kamani.

Nao baadhi ya vijana waliohudhuria mafunzo yaliyofanyika nchini Uganda kwa ajili ya Kupata mafunzo ya kuongeza uwezo na ufanisi katika kuhudumia uleaji na ukuzaji wa viumbe maji kwa njia ya vizimba.

Wamesema kuwa vitu walivyojifunza ni pamoja na utotoleshaji wa vifaranga vya kambale na Sato,utengenezaji wa chakula Cha samaki,ukarabati wa vizimba kabla,usalama wa mazingira katika kazi, utafiti wa Kupata chanzo mbadala Cha protein,kuhudumia kizimba mazingira salama,kuchakata samaki.

Jumla ya watu 281 wamepata mafunzo ya ufugaji samaki kwa njia ya Vizimba  ambapo Vijana ni 202 na watu binafsi ni 79.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma