Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amewataka vijana Mkoani Mwanza kuchangamkia fursa za fedha ambazo Serikali ya awamu ya sita inatoa kwa ajili ya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu.
Wito huo umetolewa katika kikao Cha UVCCM mkoa wa Mwanza cha Baraza la kikanuni ambacho kimefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya jiji la Mwanza na kusema kuwa vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kulitea taifa maendeleo katika kujituma kufanya kazi kwa bidii.
Eng Gabriel amesema kuwa vijana Mkoani hapa wametakiwa kuchangamkia fursa ambazo zitawakwamua kiuchumi pamoja na kimaendeleo.
Aidha ametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupokea tuzo nchini Ghana na kuiletea heshima taifa pamoja na Vijana UVCCM Mkoa wa Mwanza wametambua uongozi wa taifa na kumpa heshima mwenyekiti wa chama taifa Kama kiongozi wa kimapinduzi kwenye zama hizi na kuwaomba vijana waendelee kuwa na uzalendo katika taifa la Tanzania na kutanguliza taifa mbele.

Akizungumza fedha za mikopo bilion 8.9 ambayo ilitengwa kwa ajili ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambayo bilion 4.9 ilikuwa haijarudishwa kwa kipindi Cha miaka mitatu hivyo makundi hayo maalumu yametengewa na serikali 10%ya fedha kwa mgawanyo wa nne nne mbili ili waweze kuingia kwenye fursa za kujiongezea kipato.
“Utaratibu ulikuwa na changamoto sababu niliona watu wasiostahili wamepewa hizo fedha,baadhi ya watumishi wa halmashauri pamoja na wenye ajira wamechukua hizo fedha nimetembelea halmashauri zote nilianza kuelimisha juu ya kanuni 24 zinazosimamia mikopo na nimetoa mwezi mmoja watu ambao hawatajitokeza tutaanza kuwasaka ili tujue ni nani alizochukua hizo fedha wajitokeze kulipa madeni fedha zirudi ili kuwasaidia vijana wengine katika kuanzisha biashara Jana nimepokea kiasi cha shilingi milioni 680 za Mkopo kwa ajili ya vijana,wanawake na watu wenye ulemavu “amesema RC Gabriel.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Jonas Rufungulo amesema kuwa Mkoa wa Mwanza umepata fursa katika vyuo 32 ambayo vinajengwa nchi nzima vyuo 2 vinajengwa katika Wilaya ya ukerewe na Kwimba hivyo itasaidia vijana kutumia vyuo hivyo kwa ajili ya fursa za kujiajiri wenyewe.
“Tunampongeza Rais Samia kujenga madarasa shule za msingi mpaka Sasa wanafunzi wetu hawakai chini,hatuna mwanafunzi anayeacha kwenda shule,pamoja na vijana kupewa 4% ya mapato ya halmashauri” amesema Rufungulo.
Nae mmoja wa wahamasishaji wa boda boda Abdalla ( Dullah Kibajaji) mwana chama wa CCM amesema kuwa Rais Samia amewasaidia boda boda wametambulika Kama maafisa usafirishaji.
Aidha amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwakumbuka vijana wa bodaboda ambao wamekuwa ni Chachu katika kuleta maendeleo ya Taifa.