skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Anita Balingilaki, Itilima

Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM wamehimizwa kutokaa kimya badala yake watangaze na kunungumzia mafanikio mbalimbali ya utekelezaji wa Ilani ya Chama chao ikiwemo kuitaja miradi inayotekelezwa katika jamii kote nchini ii wananchi wafahamu bayani namna serikali inavyotekeleza matakwa ya chama.

Rai hiyo imetolewa na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu ndugu Athuman Salaga wakati akihutubia vijana kwenye kikao cha baraza la umoja wa vijana wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.

Comrade Salaga amesema miongoni mwa majukumu ya umoja huo (UVCCM) ni kuwaambia wananchi mazuri na makubwa yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na serikali inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan.

Ameongeza kuwa wilaya hiyo kwa kipindi cha uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imepata fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo ikiwemo miradi ya afya, elimu,maji barabara na umeme na miongoni mwa fedha hizo ni zaidi ya shilingi milioni 300 ambazo zimetumika kwenye ujenzi wa barabara zenye urefu wa zaidi ya km 300 wilayani hapo.

Katibu wa UVCCM mkoa wa Simiyu Athuman Salaga akiongeza na wajumbe wa baraza

“Tunashuhudia zaidi ya shilingi milioni 200 zimetumika katika ujenzi wa kituo cha afya Kanadi, zaidi ya milioni 50 zimetumika kwenye ujenzi wa zahanati ya Mwalali, katika elimu pia ameleta zaidi ya bilioni 1.4 kwaajili ya utekelezaji wa elimu bure katika wilaya hii (Itilima) hizi zote ni jitihada za Rais wetu mpendwa kwa watanzania, Rais wetu mpendwa amefanya mengi tukianza kuyaorodhesha hapa hatuwezi kumaliza”

Amesema Salaga

kwa upande wake Comrade Elias Nyasilu ambaye ni katibu wa chipukizi mkoa wa Simiyu amesema awamu ya sita inafanya kazi kubwa kwenye miradi mingi ya maendeleo ambayo inawanufaisha wananchi moja kwa moja.

” Hii awamu ya sita ya mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan inafanya kazi kubwa, zipo fedha nyingi zimeletwa na zinaletwa za miradi ya maendeleo kwenye halmashauri zetu , ndugu zangu ni mabilioni yanaletwa kwenye halmashauri zetu kwaajili ya miradi ya maendeleo”

amesema Nyasilu.

Aidha Nyasilu amesema fedha hizo zimepelekwa moja kwa moja kwenye miradi ya maendeleo huku akitolea mfano kuwa ni ujenzi wa muindombinu ya maji, umeme,zahanati, hospitali na sekta nyingine nyingi.

Awali mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) wilaya ya Itilima Kidima Himbo amewataka viongozi hao mara baada ya kutoka kwenye baraza hilo wakawe mbegu ya kuyasemea mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye kata na vijiji vyao

Wakiongea kwa niaba ya wajumbe wa baraza hilo Kalisanya Hilu ambaye ni katibu wa hamasa kata ya Mwalushu na Bahati Nshashi katibu wa hamasa kata ya Luguru wamesema wamepokea maelekezo yote na wanaenda kuyafanyia kazi.

Kikao hicho cha baraza kimewahusisha viongozi wa chama hicho ngazi ya mkoa na kata 22 zilizopo wilayani Itilima wakiwemo wenyeviti, makatibu na chipukizi .

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma