skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Anita Balingilaki, Simiyu

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limebaini kuwepo kwa uwezekano wa kupatikana kwa mafuta katika bonde la Eyasi wembere linalohusisha mikoa mitano ya Arusha, Singida, Tabora, Shinyanga na Simiyu.

Hayo yamebainishwa mapema leo na Meneja mradi wa utafiti mafuta na gesi katika bonde la Eyasi Wembere Sindi Maduhu wakati akitoa taarifa ya ufatiliaji wa mafuta na gesi asilia katika bonde la Eyasi Wembere kwenye kikao baina ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Simiyu lengo likiwa kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya utafiti.

Bw. Maduhu amesema tayari sampuli 1,136 zimepelekwa nchini marekani ili kuchakatwa na hatimaye kuangalia kama kuna viashiria vya mafuta kwenye maeneo ya mikoa mitano hiyo.

Awali akifungua kikao hicho mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amesema ni jambo kubwa mhe,Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea kufungua nchi huku akiongeza kuwa utafiti huo ukileta matunda itakuwa ni neema kwa mkoa huo na mikoa mingine inayopitiwa na bonde hilo.

“Itakuwa ni faida kwa watanzania wote maisha ya wananchi wetu yataendelea kuchangamka hii tunaiona ni fursa kubwa kwenye mkoa wetu wa Simiyu “Dkt Nawanda.

Kwa upande wake meneja uhusiano na mawasiliano kutoka TPDC Marie Msellem amesema watakapofikia muda wa kufanya kazi ni vyema wananchi wa eneo husika wakachangamkia fursa zilizopo ili kujiongezea kupato

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma