skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Shirika la maendeleo la Uswiss SDC kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na Utamaduni UNESCO wametoa msaada wa vifaa vya utangazaji vyenye thamani ya shilingi milioni 400 kwa vituo 16 vya Radio ambavyo ni mwanachama wa Mtandano wa Radio za Kijamii nchini Tanzania

Akikabidhi vifaa hivyo kwa mwenyekiti wa mtandao huo ndugu Prosper Kwigize, Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa UNESCO Tanzania Bw. Tirso Dos Santos akifuatana na afisa miradi wa SDC Eric Kilunga, wamesema kuwa dhamira ya serikali ya Uswiss na Unesco ni kujengea uwezo Radio za Kijamii kutoa huduma stahiki kwa wananchi hususani vijijini sambamba na kukuza wigo wa upashanaji wa habari

Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Mh. Innocent Bashungwa akishirikiana na mwakilishi wa Uneso Tanzania Tirsoo dos Santos (kulia) na mwakilishi wa SDC Tanzania Eric Kalunga (kushoto) kumkabidhi mwenyekiti wa TADIO Prosper Kwigize vifaa kwa ajili ya Radio za kijamii.

Bw. Santos amebainisha kuwa UNESCO na SDC wataendelea kutoa usaidizi wa mafunzo na zana za kazi ili kuwezesha Tanzania kuwa na mazingira rafiki na huru ya upashanaji wa habari kwa kuzingatia malengo endelevu ya umoja wa mataifa, lengo namba 16 kama kipaumbele mhimu.

Kwa upande wake Rais Samia Suluhu Hassa aliyewakilishwa na waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo katika maadhimisho ya kilele cha siku ya Uhuru wa habari nchini Tanzania, Bw. Innocent Bashungwa (mbunge) ameahidi kuwa serikali itaendelea kushhirikiana na wadau wa habari nchini kutatua changamoto mbalimbali za kanuni na sheria ili kazii ya utoaji na usambazaji wa habari iwe rahisi na jamii inufaike na huduma za upashanaji wa habari.

Mheshimiwa Innocent Bashungwa Waziri wa habari, sanaa, utamaduni na Michezo akihutubia wanahabarii katika sikuu ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika kitaifa mjini Arusha.

Wakati huo huo Serikali ya Sweeden imeahidi kuongeza juhudi za kusaidia waandishi wa habari kufanya kazi zao katika mazingira salama ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wanahabari kutambua haki na fursa sambamba na mafunzo ya kujihami wawapo kazini

Ahadi hiyo imetolewa na Balozii wa Sweeden nchini Tanzania Bw. Anders Sjdberg wakati akitoa salaam za serikali ya sweeden katika kilelel cha maadhimisho ya uhuru wa habari duniani ambapo nchini Tanzania yamefanyika mkoani Arusha.

Kauli mbiu ya siku ya uhuru wa habari mwaka huu ni habari kwa manufaa ya Umma

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma