skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Uswiss SDC, linaendelea na kujenga uwezo kwa viongozi wa Shirika la Habari za Maendeleo Tanzania (TADIO) ambalo ni mwamvuli wa mtandao wa Radio za Kijamii Tanzania.

Bi. Rose Ngunangwa Mwalongo afisa mradi kutoka UNESCO akizungumza na washiriki kuhusu malengo ya mradi.

Mafunzo hayo yanayofanyika Mjini Morogoro kwa muda wa siku tano yanalenga kuwezesha Radio za kijamii kujisimamia na kutoa huduma stahiki kwa jamii hasa vijijini ambako mfumo wa upashanaji wa habari unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo hali duni ya kiuchumi na mawasiliano

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, kulia ni Cosmas Lupoja (mratibu wa shirika la TADIO) na Shaaban Makame (mweka hazina wa TADIO)

Viongozi wa shirika hilo, wanajengewa uwezo wa kufahamu masuala kiutawala, utafutaji na usimamizi wa fedha, kutambua wadau na namna ya kushirikiana na jamii katika utekelezaji wa shughuli zake.

Mwenyekiti wa shirika la uwekezaji, Utu na Maendeleo OHIDE Bw. Prosper Kwigize ambaye pia ni mwasisi na msimamizi wa mchakato wa uanzishwaji wa kituo cha Radio cha BUHA FM ni mmoja wa washiriki wa Mafunzo hayo yanayotolewa kwa awamu mbalimbali.

Ndugu Prosper Kwigize Mwenyekiti wa TADIO na Mwasisi wa BUHA FM inayotarajiwa kurusha mawimbi yake wilayani Kasulu mkoani Kigoma

Aidha Kwigize ambaye pia msimamizi mwenza wa kituo cha Mpanda Radio FM ya mkoani Katavi, ndiye mwenyekiti wa mtandao wa Radio za Kijamii Tanzania chini ya shirika la habari za maendeleo Tanzania (TADIO) ambalo shinguli zake kwa asilimia 60 zinafadhiliwa na SDC kupitia UNESCO.

Wakati wa mafunzo hayo, TADIO imefanya zoezi la kutambua wadau mhimu ambao wakitumika vema suala la upashanaji habari na ukuzaji wa shirika hilo litafanikiwa.

Mkuu wa Idara ya mahusiano na Masoko Bi. Irene Makene amewataja UNESCO, SDC, Serikali, Radio Jamii, Chuo Kikuu Huria Tanzania, VIKES Finland, Umoja wa Ulaya, We-world ya Italia, Shirika la msaada wa sheria LSF na shirika la kujenga na kuimarisha mfumo wa afya kwa umma HPSS.

Bi. Irene Makene Afisa mahusiano na Masoko wa TADIO

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma