skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Adela Madyane-Kigoma

MWAKILISHI mkazi wa mashirika ya umoja wa mataifa Zlatan Milisic amesema awamu ya pili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi kupitia mradi wa pamoja wa UN Kigoma Joint Program (KJP) utahusisha watu 400,000 kutoka wilaya zote za mkoa wa Kigoma utakaokugharimu kiasi cha dola milioni 22.5 kwa mwaka 2022-2027.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya mpango huo uliofanyika mjini Kigoma utakaotekelezwa na Mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa huku vipaumbele vyake vikiwa ni pamoja na elimu bora, afya bora, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ulinzi,amani, haki na usawa, pamoja na jinsia vinapatikana kwa ubora kwa wananchi wanaoishi maeneo karibu na makambi ya wakimbizi.

Milisic amesema kuwa Umoja wa Mataifa umeongeza utekelezaji wa mpango huo kwa miaka mingine mitano kufuatia mafanikio makubwa ambayo mpango huo imeupata katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wake na kutaka kuendelea kuboresha mafanikio hayo sambamaba na kuongeza wigo wa wanufaika.

Mwakilishi mkazi wa mashirika ya umoja wa mataifa Zlatan Milisic akitoa maoni yake juu ya utekelezaji wa mradi wa KJP awamu ya kwanza

Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye amesema kuwa amefarijika kuona awamu hii ya pili miradi imejikita katika vipaumbele vya kutatua changamoto na mahitaji yaliyopo kwa wananchi na kwamba zile huduma bora zilizokuwa zikitolewa kambini zitatolewa pia katika jamii zinazozunguka kambi ikiwemo afya bora, elimu bora, mazingira bora pamoja na kudhibiti masuala ya ukatili wa kijinsia

Kwa upande wa mkuu wa ushirikiano kutoka ubalozi wa Ireland Mags Gaynor amesema anatarajia kuona umoja na mshikamano zaidi kwa mashirika ya umoja wa mataifa ili kuongeza ufanisi katika shughuli zake na kushauri kuwa hawapaswi kupuuza changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi badala yake wajikite zaidi katika kutafuta wawekezaji watakao wekeza katika nishati mbala

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma