skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Manispaa ya kigoma ujiji imepokea mabomba ya Maji kutoka Serikalini yenye thamani ya Shilingi milioni 600 ambayo yanaanza kutandikwa katika kata kadhaa ikiwemo kata ya Bangwe.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ester Mahawe, amesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutimiza adhima ya kumtua ndoo Mama kichwani ifikapo mwaka 2025.

Aidha Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira KUWASA Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mhandisi Jonas Mbike, amesema wamejipanga kuhakikisha wanafikisha huduma ya Maji kwa wananchi ambao hawajafikiwa na huduma hiyo.

Baadhi ya wananchi Kata ya Bangwe, ambao ni miongoni mwa maeneo yatakayonufaika na utandikaji wa mabomba hayo, wameiomba KUWASA kuanza zoezi hilo mapema, ili waondokane na adha inayowakabili ya kutopata huduma ya maji safi na salama.

Katika manispaa ya kigoma Ujiji mtandao wa maji umesambaa kwa kilometa  320, na katika utafiti inaonyesha zinahitajika kilometer 120 nyingine, ambapo  kupitia mradi unaoenda kutandika ni kilometa 62 katika mwaka huu wa fedha, na kati ya hizo tayari wamepokea kilometa 18 ambapo zitakuwa zimebakia kilometa 58 pekee ambazo hazijafikiwa na mtandao huo wa Maji.

Imeandaliwa na Emmanuel Kamangu- Kigoma

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma