skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na Idd Mashaka

Timu ya taifa ya Tanzania kwa wenye ulemavu maarufu kama tembo warriors imewasili salama nchini Uturuki tayari kwa mashindano ya kombe la dunia kwa mpira wa miguu yanayotarajia kuanza September 30 mwaka huu mjini Istanbul.

Akizungumza na buha fm kocha mkuu wa timu hiyo Salvatory Edward amesema “tayari wameshawasili nchini Uturuki nakwamba timu imeanza mazoezi kwalengo la kujiweka sawa kwa ajili ya mashindano hayo ambayo nimuhinu kwa timu” .

Sambamba nahayo kocha ameongeza kuwa mazoezi yanahusisha mpango maalumu wakuzoea hali ya hewa ya nchini Uturuki ilikuweka sawa miili ya wachezaji tayari kwa mapambano

Akizungumza kuhusu maandalizi ya awali yaliyofanyika jijini Dar es Salaam wakati wa Kambi maalumu amesema “wachezaji wote kuanzia nafasi ya mtunza goli nakuendelea waliweza kufanya mazoezi kama utaratibu wa kocha ulivyokuwa umepangwa nakufanikiwa kwa asilimia kubwa”.

Timu ya taifa ya Tanzania kwa watu wenye ulemavu ikiwa katika uwanja wa mazoezi nchini Qatar ikijinoa tayari kwa mtifuano

Ramadhan Ally Chomelo akiwa nimiongoni mwa nyota wa timu hiyo amesema kwa upande wao kama wachezaji wako vizuri nawamezingatia kwa kiasi kikubwa maelekezo yote ya kocha

Warriors wameenda kushiriki mashindano hayo ikiwa ni mara baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya AFCON kwa upande wa mpira wa miguu kwa wenye ulemavu wa viungo yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam mwanzoni mwa mwaka huu.

Aidha hatua hiyo imekuja ikiwa nikufuatia jitihada mbalimbali za kuwashirikisha makundi yote katika masuala ya kijamii ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali ya awamu ya sita chini Mhe:Rais Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa vijana wanaounda kikosi cha timuu ya taifa ni waliosoma na kulelewa katika shule ya msingii mazoezii Kabanga iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma