skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Wiki Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, alihitimisha ziara ya siku nne ya kikazi katika mkoa wa Kigoma ambapo pamoja na mambo mengine alikagua miradi mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara, bandari na hospitali

pamoja na mambo mengine rais Samia aliahidii kuupa hadhi mkoa wa kigoma ili kuwa kitovu cha utoaji wa huduma za afya katika kanda ya magharibi na sehemu ya kusini mwa Ziwa tanganyika ili kuwapunguzia adha wananchi hususani wagonjwa kwenda kupata huduma za kibingwa katika hospitali ya Rufaa Bugando

Akihutubiwa wananchi katika Hodpitali ya Rufaa Maweni Kigoma, Rais Samia alikiri kuwa serikali imekuwa ikiingia gharama kubwa kuwasafirisha wagonjwa kutoka Kigoma na mikoa ya jirani kwenda kutafuta huduma katika mkoa wa Mwanza na Dar es Salaam, na kwamba serikali inakusudia kujenga hospitali ya Rufaa ya Kanda katika mkoa wa Kigoma ili kupunguza adha hiyo na kuhudumia pia nchi za jirani

Sikiliza hotuba ya Rais hapa chini

Wakati huo huo Tanzania imekusudia kuimarisha miundombinu ya usafiri na usafirishaji kati yake na nchi za jirani kwa kujenga bandari mpya za Kibirizi, Ujiji na bandari ya nchi kavuu ya Katosho ili kupanua wigo na fursa za kibiashara baina ya tanzania,, Burundi, DRC na Zambia

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Makame Mbarawa amebainisha hayo wakatii akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzii wa bandari ya Kibirizi katika fukwe za Ziwa Tanganyika mjini Kigoma ambayo ni sehemu ya Bandari kuu ya Kigoma

Mbarawa pamoja na mambo mengine ameeleza kuwa serikali inakusudia kujenga Meli kubwa ya mizigo na meli nyingine ya abiria ili kuongeza kasi ya usafirishaji wa shehena inayotoka Bandari ya Dar es salaam na tanga kwenda nchi za Burundi, DRC na Zambia kupitia reli ya katii na bandari ya Kigoma

Ziwa Tanganyika kwa sasa linakabiriwa na Ombwe kubwa la kukosa Melii za uhakikia za kusafiria na kusafirisha mizigo kwenda nchi za jirani, kufuatia Meli kongwe ya MV Liemba kuchakaa na kuhitaji marekebisho makubwa huku meli nyingine ya MV Mwongozo ikifanya kazi za utafiti wa mafuta katika ziwa hilo lenye kina kirefu barani Afrika.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma