skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Na. Mwandishi wetu – Bukoba

Sirika la Afya duniani WHO limethibitisha kumalizika kwa ugonjwa wa homa ya Marburg ambaoo uliwaua watu sita nchini Tanzania mapema mwaka huu na kuacha taharuki miongoni mwa wakazi wa ukanda wa maziwa makuu

Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu akiambatana na maafisa wa kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Marekani US CDC, kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Umoja wa Afrika Afrca CDC, WHO, UNICEF, madaktari wasio na mipaka, Amref na wadau wengine wametoa kauli hilyo mapema leo mjini Bukoba wakitthibitisha kuwa hakuna tena vizuri vya Marburg nchini Tanzania

Dr. Tumaini Nagu mganga mkuu wa serikali akitoa taarifa ya mafanikio ya kuudhibiti ugonjwa wa homa ya Marburg, wa pili kushoto ni Dr. Zabron Yoti mwakilishi wa WHO nchini Tanzania

Kufuatia kupatikana kwa mafanikio hayo Wariri Mwalimu ameshukuru jumuiya ya kimataifa hususani Umoja wa Ulaya, marekani na umoja wa Afrika kwa kutoa misaada mbalimbali iliyotumika katika mapambano hayo ikiwemo kutoiwekea vikwazo nchi hiyo

Miongoni mwa watu watatu walionusurika kifo baada ya kuambukizwa Marburg ni Mganga wa kituo cha Maruku Dr. Mahona Ndalu mbaye anatoa ushuhuda wa kilichompata na kuihimiza serikali kuweka mkakati maalumu wa kuwajengea uwezo madaktari katika eneo la tahadhari na kinga wawapo kazini

Dr. Dr. Mahona Ndulu (katikati) aliyeugua na kupona Marburg akitoa ushuhuda

Taarifa ya serikali ya Tanzania imebaiinisha kuwa pamoja na watu tisa walioambukizwa na vifo vya watu 6 mganga mkuu wa serikali serikali ya Tanzania Dr. Tumaini Nagu anataja kuwa watu Zaidi ya 200 waliathirika kwa namna mbalimbali ikiwepo kuishi maisha ya hofu, kushuka kwa uchumi na athari za kisaikolojia

Ni wapi ugonjwa huu ulitoka? Swali hili linamuumiza Waziri wa afya Ummy Mwalimu na hivyo kulazimika kutoa wito kwa watafiti wa ndani na nje kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na taasisi za utafiti wa magonjwa pamoja na chuo kikuu cha SUA kuona kama chanzo cha marburg ni virusi vilivyotokana na popo ama lah

kwa upande wake mwakilishi shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania Shalin Bahuguna amepongeza kwa namna serikali na wadau wa afya walivyoshirikiana katika kupambana na janga hilo huku akisisitiza juu ya umhimu wa kushirikisha wananchi na viongozi wa ngazi ya jamii

Shalin Bahuguna (katikati) akitoa hotuba kwa niaba ya UNICEF kwenye kilele cha mapambano dhidi ya marburg mkoani Kagera

“Nilishuhudia mwenyewe namna makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo viongozi wa jamii ngazi ya vijiji walivyotoa ushirikiano katika kupambana na marburg, hivyo natoa wito mahususi kwa wadau wote kuhakikisha kila jambo jamii na viongozi wao washirikishwe ili kupata ufanisi zaidi. Amesema Shalin

Shirika la Afya duniani kupitia kwa mwakilishi wake nchini Tanzania Dr. Zabron Yoti wametoa pongezi kwa Tanzania kwa namna serikali ilivyochukua hatua za haraka na kufanikiwa kuzuia maambukizi kutosambaa nchini Tanzania na duniani kwa ujumla

Baadhi ya wadau wa afya walioshiriki hafla ya kumalizika kwa virusi vya Marburg nchini Tanzania

Pamoja na hayo Umoja wa Afrika na chake cha udhibiti wa magonjwa Africa CDC kupitia kwa kaimu mkurugenzi wake nchini Tanzania Dr. Ahmed Ogwell Ouma pamoja na kupongeza kwa namna nchi za afrika zinavyoshirikiana, amehimiza nchi za afrika mashariki kuwa na mpango wa pamoja wa kushughulikia magonjwa ya milipuko

Ugonjwa wa Marburg umewahi kuikumba nchi ya Uganda na DRC katika nyakati tofauti na kufanikiwa kuudhibiti hali inayoziamsha taasisi za utafitii kufuatilia kwa kina kuhusu chanzo cha ugonjwa huo.

Mwandishi: Prosper Kwigize- CA habari Kagera

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma