Na. Mwandishi wetu, Kinshasa DRC Wakati Kanisa Katoliki nchini Tanzania likifanya ibada maalumu kumkumbuka Rais…
Tanzania imeadhimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika maarufu kama Tanzania bara, ikitaja kujivunia mafanikio makubwa sanakatika Nyanja za maendeleo ya jamii, ulinzi na usalama pamoja na ushiriki wa majeshi katika ulinzi wa amani katika nchi mbalimbali duniani. Mwandishi wetu prosper Kwigize ametuandalia riport ifuatayo
Katika maadhimisho ambayo yametajwa kufana, wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Rwanda, Kenya, Msumbiji, Madagascar na wengine wamehudhuria maadhimisho hayo yalioyoshereheshwa na maonesho ya zana za kijeshi ikitafsiriwa kuwa ni kuonesha ukakamavu, weledi na uwezo wa jeshi la Tanzania katika kulinda mipaka ya nchi hiyo.
Rais Samia Suluhu hassan analipongeza jeshi hilo kwa kufanikisha kuulinda uhuru na usalama wa taifa hilo la afrika mashariki linalotambulika kama kitovu cha kupiganisha uhuru wa mataifa mbalimbali kusini mwa jangwa la sahara.
Aidha mama Samia pamoja na kulisifu jesshi anataja tanzani akuapat amafanikio makubwa katika sekta mbalimbali za kijamii, kisiasa, kiuchumi na mahusiano ya kimataifa.
Wananchi wa Tanzania wamekuwa na maoni mbalimbali kuhusiana na miaka sitini ya uhuru wa Tanzania bara. Gaudence Gwinjira ni mkufunzi wa chuo cha ualimu Sumbawanga kusini magharibi wa Tanzania
Tanzania inapoadhimisha miaka sitini ya uhuru wa Tanganyika iliyoungana na visiwa vya Unguja na pemba na kuunda taifa la Tanzania inatajwa kukua kiuchumi na kuufikia uchumi wa kati wa daraja la chini.
SIKILIZA HOTUBA YA RAIS WA HAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMA SAMIA SULUHU HASSAN- BOFYA HAPO CHINI.
Hongera Tanzania
Prosper Kwigize