Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua Kamati ya…
Serikali za Tanzania na Kenya zimefanya makubaliano ya kupunguza ama kuondoa vikwazo vya kibiashara ambavyo vimekuwa vikikwamisha ukuaji wa uchumi kwa pande zote mbili na pia kuyumbisha mahusiano ya kiuchumi na kidiplomasia baina yao
Kwa mujibu wa mtandaoo wa matokeo chanya, Waziri wa viwanda na biashara Prof Kitila Mkumbo amewahimiza wafanya biashara wa pande zote mbili kuanza kufanya uwekezaji na kuendeleza biashara zao.
Hayo ameyasema katika Mkutano wa tano (5) baina ya Tanzania na Kenya kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya biashara ikiwemo vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru (NTBs) baina ya nchi hizo uliofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Mei 2021 katika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha, ikiwa ni siku chache tangu marais wa Kenya na Tanzania walipokutana na kujadiliana kuhusu ujirani mwema, uchumi na biashara.
Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania Prof. Kitila Mkumbo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Wajasiliamali nchini Kenya, Mhe. Betty Maina na ujumbe kutoka hizo nchi mbili wakiwa majidiliano ya masuala mbalimbali ya biashara ikiwemo kuondoa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru baina ya nchi ya Tanzania na Kenya katika kikoa kilichofanyika ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC) jijini Arusha, 29 Mei 2021.
Katika mkutano huo Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Mkumbo ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano huo ambao ulijumuisha Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, wakati ujumbe wa kenya ukiongozwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Maendeleo ya Wajasiliamali Mhe. Betty Maina aliyeambana na Balonzi wa Kenya nchini Tanania