skip to Main Content
Simu: +255 653 200 211 | Barua Pepe: info@buhafmradio.co.tz  

Serikali za Burundi na Tanzania zimekubaliana kuongeza ushirikiano Zaidi katika Nyanja za ulinzi na usalama, uchumi na mahusiano ya kijamii ili kuharakisha maendeleo ya Burundi ambayo imekuwa katika hali duni ya kiusalama kwa muda mrefu.

Maazimio hayo yanafanyika katika mkutano wa ujirani mwema baina ya Mkoa wa Kigomana Katavi pamoja na mikoa mitano ya Burundi inayopakana na Tanzania unaofanyika mjini Kigoma magharibi mwa Tanzania

Mkuu wa Mkoa wa Makamba nchini Burundi Francoise Ngozirazana ambaye ni mwenyekiti wa mkutano wa ujirani mwema akihutubia katika mkutano uliofanyika mjini Kigoma leo.

Akizungumza kuhusu maazimio mbalimbali ya vikao vya ujirani mwema, mkuu wa mkoa wa Makamba nchini Burundi Bi. Francoise Ngozirazana ambaye ni mwenyekiti wa mkutano huo, ameipongeza Tanzania kwa namna inavyoshirikiana na Burundi kuimarisha ulinzi na kutokomeza uhalifu mpakani

Bi Francoise amehimiza pia juu ya makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa katika azimio la mmwaka 2017,2019, 2020 na yale ya hivi karibuni yam waka 2022 kuhusu kurejesha wakimbizi wa Burundi nchini mwao kwa hiyari na kuongeza mpango wa wakimbizi kupelekwa Burundi kujionea hali ya amani uliopewa jina la “Nenda kajionee” ambapo wakimbizi 18 wakiambatana na maafisa wa UNHCR na serikali ya Tanzania walizuru Burundi na kujionea hali ya amani na usalama

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amepongeza ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Burundi hasa katika sekta ya ulinzi na Uchumi, akisisitiza kuwa mpango wa ujirani mwema unazisaidia pande zote mbili

Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukamilika kwa mkutano wa ujirani mwema. walioketii kutoka kulia ni Reverien Ndukuriyo katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD chini Burundi, Bi. Francoise Ngozirazana mkuu wa mkoa wa Makamba nchini Burundi, Thobias Andengenye mkuu wa mkoa wa Kigoma Tanzania na Kaimu katibu tawala mkoa wa Kigoma.

Wakati huo huo Katibu mkuu wa chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD Reverian Ndikuriyo amezipongeza pande zote mbili za Tanzania na Burundi kwa kuendeleza mpangoo wa ujirani mwema ambao aliuasisi yeye akiwa mkuu wa mkoa wa Makamba nchini Burundi  miaka 18 iliyopita, huku akisisitiza kuhusu kuongeza ushirikiano wa kijamii kupitia sekta ya michezo katika mashindano ya Kombe la Tanganyika kwa kushirikiasha wanafunzi wa shule za msingi ili kuibua vipaji

Hivi Karibuni serikali ya Tanzania na Burundi zilitiliana saini kuanza kutekeleza miradi ya pamoja ya ujenzi wa reli kutoka Kigoma hadi Musongati mkoani Rutana nchini Burundi pamoja na kuimarisha shughuli za usafiri wa Anga na majini kupitia ziwa Tanganyika.

Back To Top
Buha FM · Buha FM Radio Sauti Ya Kigoma