Asema ni mpango wa kumtua mama kuni kichwani , Amshukuru Rais Samia Na. Mwandishi wetu…
Adela Madyane- Kigoma
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoani Kigoma imefanikiwa kuokoa zaidi ya milioni 58 katika kipindi cha robo ya tatu kuanzia mwezi Julai mpaka September 2022 kutokana na kushughulikia malalamiko mbalimbali yaliyofanyiwa uchunguzi yakiwemo ya taarifa 36 zinazohusu rushwa.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kwa niaba ya kamanda wa TAKUKURU mkoa, John Mgallah Naibu Mkuu wa TAKUKURU Kigoma amesema wamefanikiwa kuokoa zaidi ya milioni 14 kati ya 69 ambazo zilitolewa na serikali kuu kwaajili ya kulipia nauli za likizo za walimu wa shule za mzingi katika halmashauri ya wilaya ya Kigoma mnamo Agosti 2022.
“Milioni 10,438,400 ziliokolewa kutoka kwenye matumizi yasiyo sahihi ambazo zilipunjwa kutoka kwenye fedha za malipo ya likizo ya walimu huku milioni 4, 690,000 zilibainika kuchepushwa kutoka kwenye malipo hayo na kulipwa kama posho kwa watumishi wa halmashauri wanaodaiwa kufanya uchambuzi” Amefafanua Mgallah

Sambamba na hilo tasisi hiyo katika halmashauri ya wilaya ya Kasulu imeweza kuokoa zaidi ya milioni 43 kati ya milioni 420,000,000 zilizochepushwa na watumishi wasio waadilifu kwaajili ya matumizi yao binafsi kutoka katika pesa za wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) kwa vijiji 61 vya wilaya hiyo kati ya mwezi Mei na Juni 2022.
“Baadhi wafanyakazi wanaotekeleza mpango huo wakiwemo wa idara ya fedha walitengeneza mtandao wa kupunguza kiasi cha fedha kutoka kwa wanufaika wa mpango wa TASAF, kama mnufaike alistahili kulipwa elfu 50,000 wao walikata pesa na kumlipa elfu 20,000 kinyume na mwongozo wa taasisi husika ndo maana tumeweza kuokoa kiwango hicho cha pesa” Ameeleza Naibu Mkuu
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mgallah, amesema uchunguzi wa makosa hayo bado unaendela ili kuwafikisha washtakiwa mahakamani na kwamba katika kipindi hicho wameweza kufanya ufuatiliaji kwenye miradi ya maendeleo 17 yenye thamani ya bilioni 6.9 katika sekta za maji, elimu, barabara na afya.