Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:…
Na. Anita Balingilaki na Prosper Kwigize, Bariadi
Katika kudhibiti ugonjwa wa kifua kikuu na magonjwa mengine ya kuambukiza, serikali imetoa vifaa mbalimbali vya vipimo, kinga na tiba katika mikoa mbalimbali ili jamii ipate huduma inayostahili
katika mkakati huo Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa ambayo tayari imepokea vifaa vya kisasa vitakavyotumika kutekeleza afua za afya ya jamii pamoja na tiba ya ugonjwa wa kifua kikuu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amebainisha hayo wakati akitoa taarifa ya mkoa kwa Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na kifua kikuu ambayo kitaifa yamefanyika katika Mji wa Bariadi mkoani SImiyu.
Dkt. Nawanda amesema mkoa huo umepokea mashine nane za kupima vinasaba vya vimelea vya kifua kikuu ambavyo vitasaidia kuwatambua wenye maambukizi ya ugonjwa huo na kuwapa fursa matabibu kuanza kutoa huduma za haraka kwa wagonjwa watakaobainika.
Video hii hapa chini inafafanua kwa kina kuhusu namna mkoa wa Simiyu ulivyojipanga
Kwa upande wake waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kote nchini kujitokeza kwenda kupima afya zao ili kuja kama wamepata maambukizi ya kifua kikuu na kisha kuanza kupata matibabu kwa watakaobainika kuambukizwa.
Aidha majaliwa amewapongeza wataalamu, watafiti na madaktari kwa namna wanavyotimiza wakibu wao katika kuhakikisha kuwa ugonjwa wa kifua kikuu na magonjwa mengine yanadhibitiwa.

Katika hatua nyingine Waziri mkuu majaliwa amekagua maonesho mbalimbali yanayoashiria dhamira ya serikali na taifa katika kupambana na magonjwa ya kuambukiza ikiwemo gari maalumu lenye mitambo mahususi kwa ajili ya kutoa huduma za uhkiki wa afya na kutambua maambukizi

Wakati huohuo Waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameanza ziara ya siku tatu ya kutembelea mkoa wa Simiyu ambapo atazuru wilaya zote za mkoa huo, akikagua na kutembelea miradi mbalimbali ya kiuchumi, Afya na miundombinu ikiwemo reli ya kisasa ya SGR katika eneo la Malampaka kwenda Mwanza.